Kono, Waziri anayezungumza moja kwa moja kwenye mitandao ya kijamii juu ya chanjo, anakabiliwa na ushindani kutoka kwa wagombea wengine watatu, ambao wataweza kulazimisha kura ya marudio ambayo inaweza kuwa isiyo na uhakika zaidi.
Waziri Mkuu wa sasa Yoshihide Suga, mwanzoni mwa mwezi huu alitangaza kwamba atajiuzulu, baada ya kutumikia nafasi hiyo kwa mwaka mzima, kufuatia umma kutopendezwa na namna serikali inavyoshughulikia suala la virusi vya Corona.
Kujiuzulu kwa Suga kunaongeza uwezekano kwamba Japan, itarudi katika kipindi cha mawaziri wakuu wanaojirudia, jambo ambalo liliashiria miongo kadhaa iliyopita.
Kile kinachoonekana kwa karibu zaidi ni kwamba Waziri mkuu ajaye wa Japan, atatoka kwenye chama tawala cha Liberal Democratic Party (LDP).