Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:17

Rais wa Somalia amuondolea madaraka Waziri Mkuu


Rais wa Somalia amuondolea madaraka Waziri Mkuu
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:30 0:00

Rais wa Somalia amuondolea madaraka Waziri Mkuu

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo amesema amemuondolea madaraka ya Waziri Mkuu Mohamed Hussein Roble.

Rais amemshutumu Waziri Mkuu kwa kutokuwa na uhusiano mzuri wa kikazi na yeye pamoja na kufanya maamuzi ya haraka.

Ofisi ya Waziri Mkuu bado haijasema lolote kuhusu hatua hiyo. Viongozi hao wawili hivi karibuni wametofautiana kuhusu kesi ya kupotea afisa wa kijasusi Ikran Tahlil Farah.

Shirika la kitaifa la ujasusi lililomwajiri Farah limesema aliangukia kwenye mikono ya wanamgambo wa al Shabaab na kuuliwa.

Hata hivyo al Shabaab imekanusha shutuma hizo. Farah alipotea Juni 26.

Roble aliamuru mahakama ya kijeshi kufanya uchunguzi dhidi ya kesi hiyo na amemteuwa mkurugenzi mpya wa shirika la ujasusi, na Rais alipinga uteuzi huo uliofanywa na Waziri Mkuu.

Katika mvutano huo Waziri Mkuu aliikataa tume ya uchunguzi iliyoteuliwa na Rais kwa ajili ya kesi hiyo, akisema kitengo cha sheria katika serikali kiko huru mbali na mamlaka ya utendaji kwa mujibu wa Katiba ya Somalia.

Katika taarifa yake leo Alhamisi Farmajo amesema uamuzi wa hivi karibuni wa waziri mkuu unaweza kuliingiza taifa katika mzozo wa kisiasa na usalama.

XS
SM
MD
LG