Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 16:48

Upinzani walalamikia mpango mpya wa uchaguzi Somalia


Wabunbge wa Somalia wapiga kura bungeni kwenye picha ya awali
Wabunbge wa Somalia wapiga kura bungeni kwenye picha ya awali

Baadhi ya wagombea wa urais kutoka vyama vya upinzani nchini Somalia wamekataa mpango wa uchaguzi mkuu kutoka kwa serikali, ikiwa na maana kwamba huenda zoezi hilo likacheleweshwa tena.

Baraza la wagombea urais nchini humo maarufu kama CPS, Jumatatu limetoa taarifa kwamba limekataa mpango mpya wa uchaguzi uliotolewa na serikali kuu pamoja na viongozi wa kidini.

Upinzani umesema kuwa mpango huo unatoa nguvu zaidi kwa viongozi watano wa majimbo katika kuchagua wajumbe ambao hatimaye watachagua wabunge 275.

Hassan Sheikh Mohamud ambaye ni kiongozi wa upinzani anasema kuwa lazima kuwe na mchakato unaoeleweka kuhusiana ni nani atakaye chagua wajumbe, na ni nani wanaye mwakilisha bungeni chini ya mfumo wa 4.5.

Mfumo wa 4.5 unaelezea namna koo zinavyo gawana madaraka. Uchaguzi usiyo wa moja kwa moja wa wabunge umepangwa kufanyika mapema mwezi ujao kabla ya uchaguzi wa rais hapo Oktoba 10.

Hata hivyo wachambuzi wanasema kuwa huenda uchaguzi wa rais ukacheleweshwa iwapo mgogoro uliyoko hautatatuliwa kwa haraka.

Uchaguzi wa Somalia mwanzoni ulipangwa kufanyika mwaka uliyopita, lakini umecheleweshwa mara kadhaa kutokana na migogoro ya kisiasa licha ya shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Mwezi Aprili, wabunge wa Somalia walipiga kura ya kuongezwa kwa muhula wa kuhudumu wa rais lakini uamuzi huo ukabatilishwa mwezi uliyofuata. Hatua hiyo ilifikiwa baada ya ghasia kuzuka kati ya wafuasi wa upinzani na wale wa serikali kwenye mji mkuu wa Mogadishu

XS
SM
MD
LG