Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:07

Somalia yathibitisha operesheni zake zimewauwa al-Shabaab


Wanawake Somalia wakipinga tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika (AMISOM) nje ya Hospitali ya Erdogan baada ya mauaji ya raia kufuatia mapigano ya bundaki kati ya AMISOM na wapiganaji wa al-Shabaab
katika mkoa wa Lower Shabelle, Mogadishu, Somalia, Agosti 12, 2021. REUTERS/
Wanawake Somalia wakipinga tume ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika (AMISOM) nje ya Hospitali ya Erdogan baada ya mauaji ya raia kufuatia mapigano ya bundaki kati ya AMISOM na wapiganaji wa al-Shabaab katika mkoa wa Lower Shabelle, Mogadishu, Somalia, Agosti 12, 2021. REUTERS/

Serikali ya Somalia imesema operesheni za pamoja zilizofanywa na jeshi na maafisa wa usalama katika mikoa ya katikati imesababisha vifo vya wanamgambo wa al-Shabaab, vyombo vya habari vya shirika la Nation nchini Kenya vimeripoti.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Habari hii imetokea baada ya mapigano ya Jumanne na Jumatano yaliyosababisha vifo vya wapiganaji watano wa jimbo la Galmudug walioshirikiana na serikali kuu.

Taarifa imesema miongoni mwa waliokufa ni pamoja na kamanda wa kikosi cha Galmudug, Mohamed Ali na sehemu kubwa ya mapigano yalifanyika katika kijiji cha Aad kwenye mkoa wa Mudug.

Zaidi ya miezi miwili jeshi la Somalia limefanya kazi pamoja na wanajeshi wa jimbo la Galmudug kuongeza nguvu dhidi ya mashambulizi katika ngome ya al-Shabaab yenye mkoa wa Mugug na kukamata miji muhimu ya Badween na Qayad.

Vikosi hivyo vinasogea karibu na Haradere eneo maarufu la zamani la maharamia wa Somalia, lakini hivi karibuni lilishikiliwa na kundi la al-Shabaab lenye uhusiano na al-Qaida.

Jumatatu serikali ya Somalia ilisema kwamba operesheni zake miezi iliyopita ziliuwa mamia ya wanamgambo wenye msimamo mkali wa jihad. Haya yote yanajitokeza Somalia wakati nchi inajiandaa na uchaguzi mkuu wa urais.

XS
SM
MD
LG