Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:47

Uchaguzi wa bunge Somalia wacheleweshwa tena


Wakazi wa Somalia wakusanyika kutokana na mgogoro kati ya serikali na upinzani katika siku za nyuma.
Wakazi wa Somalia wakusanyika kutokana na mgogoro kati ya serikali na upinzani katika siku za nyuma.

Uchaguzi wa Somali wa wabunge usiyo wa moja kwa moja uliyotarajiwa kuanza Jumapili umecheleweshwa kwa mara ya pili kutokana na kuwa mabunge ya majimbo kutokuwa tayari.

Kuna hofu kwamba kucheleshwa zaidi kwa zoezi hilo huenda kukahatarisha uthabiti wa kisiasa wa taifa hilo. Kufikia Jumatatu, hakuna tarehe mpya ya uchaguzi wa bunge iliyo tangazwa baada ya kuahirishwa Jumapili.

Kamati ya serikali kuu inayosimamia uchaguzi huo imesema kuwa zoezi hilo lilicheleweshwa baada ya viongozi wa majimbo matano kuchelewa kuwasilisha orodha ya mwisho ya wagombea. Kamati hiyo pia imesema kuwa hakukubuniwa kamati za kieneo za kusimamia uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya uchaguzi Mohamed Hassan Irro amesema mikakati ya kuendelea na zoezi hilo bado ipo licha ya kucheleweshwa.

Uchaguzi wa rais na bunge wa Somalia ulikuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa muhula wa rais Mohamed Abdullahi Farmajo mwezi Februari , lakini migogoro kati ya serikali na upinzani ikasababisha kucheleweshwa kwa miezi kadhaa.

Upinzani hata hivyo unasema kuwa unatarajia kuwa zoezi hilo litaendelea bila matatizo katika wiki zijazo licha ya kucheleweshwa kulingana na Mohamed Hassan Idris ambaye ni mbunge kutoka upinzani na ambaye anagombea tena katika jimbo la Jubbaland.

Zaidi ya wagombea 15 tayari wametangaza nia ya kugombea urais dhidi ya Farmajo kwenye uchaguzi uliyopangwa kufanyika Oktoba 10, na ambao utapigiwa kura na wabunge 329 .

Katika taarifa nyingine ni kwamba kundi la kigaidi la al Shabab linalofanyia opereseheni zake nchini humo, na lililovuruga uchaguzi wa 2017, limeonya wajumbe kutoshiriki kwenye uchaguzi wa ubunge na urais mwaka huu.

XS
SM
MD
LG