Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 23:06

Jeshi Uganda lawakamata watoto na wanawake katika uchunguzi wa jaribio la kujilipua


Ramani ya Uganda
Ramani ya Uganda

Watoto wenye umri wa miaka mitatu na wanawake wamekamatwa katika uvamizi wa kijeshi katika Wilaya ya Wakiso kutokana na kukamatwa kwa anayedaiwa alikuwa mlipuaji bomu wa kujitoa muhanga katika wilaya ya Pader nchini Uganda.

Uvamizi huo wa Alhamisi usiku ulihusisha kukamatwa kwa watoto watatu na wanawake wawili wa familia moja pamoja na wanaume wengine waliochukuliwa kutoka nyumba mbalimbali katika maeneo ya Masajja Kibira B, Makindye, Ssabagabo Wilaya ya Wakiso.

Wanawake ho na watoto ni familia ya Imam wa Kituo cha Kiislam cha Swab – Kibira, Sheikh Ismail Mutumba.

Wakati uvamizi huo uliofanyika saa saba usiku, iliripotiwa kuwa Imam alikuwa kaitka moja nyumba zake nyingine huko Zana.

Hafitha Noowa, dada wa Kasemire Salha na mke wa Imaam, amesema alikuwa amepewa taarifa ya tukio hilo na rafiki yake.

Dada yake Kasemire, amesema alichukuliwa pamoja na binti yake Ruwah Mutumba, miaka 3, Sabika Mutumba, miaka 4, na binti mkubwa mwengine Shamusa Mutumba (wa mwanamke mwengine ambaye analelewa na Kasemire), na mfanyakazi wa nyumbani ambaye hakutambuliwa.

“Hatujui iwapo wanajeshi hao waliilenga familia nzima kwa sababu wakati walipofika katika operesheni hiyo Imaam alikuwa yuko katika nyumba yake nyingine. Tuliambiwa baada ya kukamatwa, walichukuliwa katika [gari aina ya Toyota mini Van],” Noowa alisema.

Msemaji wa Jeshi na Ulinzi, Brig Flavia Byekwaso, amethibitisha ukamataji huo, akisema unahusiana na anayedaiwa kuwa mlipuaji bomu wa kujitoa muhanga, Abdul Katumba, maarufu Ben, ambaye aliripotiwa aligundulika ana fulana ya kujitoa muhanga na vifaa mbalimbali vinavyoweza kutumiwa kutengeneza vilipuzi.

Katumba, jeshi limesema Agosti 27, alikuwa ana mpango wa kulipua bomu katika maziko ya Naibu mkuu wa polisi wa zamani, Lt Gen Paul Lokech, aliyefariki kutokana na damu kuganda hapo Agosti 21. Lokech alikuwa kamanda wa ngazi ya juu wa zamani, aliyepewa jina la Simba wa Mogadishu kwa uongozi wake thabiti nchini Somalia.

Katika mahojiano ya Jumamosi na Brig Byakwaso, alisisitiza “tutawatafuta washukiwa wote wa kigaidi na kuwakamata.”

“Humkamati mtu ukaishia hapo, bila shaka (Katumba) hakuwa peke yake. Watatakiwa kuwatafuta wale wote wanaohusika na mtuhumiwa huyu. Kamatakamata (ya Alhamisi) ni moja ya operesheni hizo,” Byekwaso amesema. Alisema hakuwa na taarifa ya watoto na wanawake waliowekwa rumande.

XS
SM
MD
LG