Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 00:12

Sudan Kusini yawasaka majambazi wanaouwa na kutishia madereva


Ramani ya Uganda- Sudan Kusini
Ramani ya Uganda- Sudan Kusini

Mamlaka Sudan Kusini imesema imetuma timu ya pamoja ya usalama kuyatafuta maeneo ambapo majambazi wanaotishia madereva wa Kenya na Uganda wanajificha kwenye barabara kuu inayotoka Uganda.

Zoezi hili limekuja siku moja baada ya madereva wa malori kusimamisha huduma za usafirishaji wa mizigo kwenda Sudan Kusini baada ya madereva wake wawili kuuwawa na magari kuchomwa moto na wahalifu wasiojulikana Jumamosi katika barabara kuu ya Juba na Nimule.

Msemaji wa polisi wa Sudan Kusini Jenerali Daniel Justine amesema jopo la pamoja la usalama ni pamoja na maafisa wa ujasusi wa kijeshi na maafisa wa polisi, ambao walionekana Jumatatu wakisaka majambazi.

Baada ya kukutana na wanadiplomasia wa Kenya huko Juba naibu Waziri wa Mambo ya Nje Deng Dau Deng ameahidi kuwepo kwa hali ya usalama kwa madereva wa kigeni.

Jumatatu chama cha wasafirishaji wa Kenya KTA kilisitisha usafirishaji wa mizigo kwenda sudan kusini baada ya madereva wawili wa malori kuuwawa kilomita 45 kutoka Juba Jumapili usiku.

XS
SM
MD
LG