Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 15:18

Serikali : Waganda kulipia rasmi huduma ya vipimo vya COVID-19


Wasafiri wakiwekewa sanitizer kabla ya kupanda mabasi katika kituo cha basi mjini Kampala, Uganda ikiwa ni kujilinda na virusi vya corona, Machi 24, 2020.Picture taken March 24, 2020. REUTERS/Abubaker Lubowa NO RESALES. NO ARCHIVES
Wasafiri wakiwekewa sanitizer kabla ya kupanda mabasi katika kituo cha basi mjini Kampala, Uganda ikiwa ni kujilinda na virusi vya corona, Machi 24, 2020.Picture taken March 24, 2020. REUTERS/Abubaker Lubowa NO RESALES. NO ARCHIVES

Wananchi wa Uganda watalipa shilingi 240,000 za Uganda ($65) kwa ajili ya kipimo cha COVID-19 wakati serikali ikisimamia gharama hizo katika hatua ya kukabiliana na janga hilo.

Waraka wa serikali kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Geoffrey Sseremba amesema, “ Huu ni utaratibu wa kuokoa gharama ambao utaiwezesha Wizara ya Afya kununua vifaa zaidi vya kupimia ili kuendelea kufanya huduma hii ya upimaji kufikiwa nchini kote.”

Lakini wananchi wa Uganda, hata hivo, wanahoji hatua hii, wakiwa wanatafakari kiwango kikubwa cha fedha ambazo nchi imepokea katika miezi mitano iliyopita kwa ajili ya kudhibiti virusi hivyo. Kuna wasiwasi kwamba upimaji huu utawatenga maskini ambao hawawezi kulipa gharama hii.

Malipo haya ni kwa yeyote anayetaka kupimwa COVID-19, lakini serikali imeorodhesha wale ambao lazima wafanyiwe vipimo.

Walioorodheshwa ni madereva wa malori, watu binafsi wanaotaka kujua hali zao, raia wa Uganda wanaorejea kutoka nje, taasisi zinazotaka kuwapima wafanyakazi wake, na wageni wanaowasili nchini. Vifaa vya upimaji 200,000 vilitolewa msaada na Taasisi ya Jack Ma.

Wadau wa maendeleo kama vile Shirika la Afya Duniani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa pia wamechangia vifaa vya kupimia. Zaidi ya vipimo 350,000 vimefanywa kwa wananchi wa Uganda nchi nzima.

Mwezi Juni, Emmanuel Katongole, ambaye anaongoza Kikosi Kazi cha Taifa kwa Covid 19, ameliambia gazeti la East African kwamba kikosi kazi kimepokea jumla ya Shilingi bilioni 33 ($ milioni 9) kati haizzo shilingi bilioni 6 (#milioni 4.3) zilikuwa fedha taslimu.

XS
SM
MD
LG