Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:35

Wanafunzi milioni 15 Uganda wana fursa finyu kielimu kufuatia COVID-19


Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Kwa miaka kadhaa ijayo, zaidi ya wanafunzi milioni 15 nchini Uganda watakuwa wanafanya juhudi kuwafikia wenzao kimasomo katika eneo la Afrika Mashariki, baada ya miezi 18 ya masharti ya kutotoka nje – na bado wakiendelea kukaa nyumbani – wakati ambapo fursa ya kufikia elimu ni finyu kama hazipo kabisa.

Ilivyo hivi sasa, serikali iko katika shinikizo la kufungua tena shule, kwanza, kwa sababu za kielimu, lakini pia ikizingatia madhara ya kiuchumi ya kufunga shule za wamiliki binafsi ambao wanakabiliwa na hatari ya mali zao kuuzwa ili waweze kulipa mikopo ya benki, limeandika gazeti la The East African, Jumapili.

Namna fulani ya kufundisha na kujifunza inaendelea katika shule binafsi za hadhi ya juu na shule za umma, ambako wazazi wanaweza kumudu gharama za vifaa, miundombinu na mawasiliano ya Wi-Fi, kuwawezesha watoto wao kusoma kwa njia ya mtandao.

Lakini shule nyingi za umma ambazo husajili wanafunzi kutoka familia maskini zimeendelea kufungwa, na tafiti kuhusu juhudi za serikali kusambaza vifaa vya masomo kwa kundi la wanafunzi hawa zinaonyesha kuwa asilimia 20 tu ya familia hizi zimeweza kupata vifaa hivyo.

Mwanafunzi wa kike akiwa karibu na njia ya reli ya Kenya-Uganda wakati shule zilipofunguliwa tena, baada ya serikali kusitisha azma yake ya kufuta muhula wa masomo kutokana na janga la COVID-19, katika eneo la Kibera, Nairobi, Kenya Octoba 2020..
Mwanafunzi wa kike akiwa karibu na njia ya reli ya Kenya-Uganda wakati shule zilipofunguliwa tena, baada ya serikali kusitisha azma yake ya kufuta muhula wa masomo kutokana na janga la COVID-19, katika eneo la Kibera, Nairobi, Kenya Octoba 2020..

Wataalam hivi sasa wanasema sekta ya elimu iko katika mgogoro wakati wahusika binafsi wanaamua namna ya kufundisha na fursa ya upatikanaji wa elimu, hali iliyoleta ukosefu mkubwa wa usawa, huku watoto wengi wa shule wakiwa wamekoseshwa aina yoyote ya masomo.

“Masomo kwa njia ya mtandao ni sawa, lakini hatukuwa tumejitayarisha kutumia njia hii. Katika sekta binafsi inaelekea tumepiga hatua za haraka kuliko serikalini – ikifanyika bila utaratibu.

Tulichukua hili kama ilivyo kwa shule binafsi ni hali ya dharura kuziba pengo lililopo, lakini linaweza kuendelezwa kwa kiwango gani? amesema Asadu Kirabira, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kitaifa ya Taasisi za Elimu Binafsi.

XS
SM
MD
LG