Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, taifa hilo la Afrika mashariki lina hitoria ya miaka mingi ya kupokea watu wanaokimbia mizozo na kwa sasa linawapa hifadhi wakimbizi wapatao milioni 1.4, wengi wao wakiwa kutoka Sudan Kusini.
Esther Anyakun Davinia, naibu wa waziri wa misaada ya dharura, majanga na Wakimbizi amesema Rais Museveni ameridhia ombi hilo lililotolewa Jumatatu na utawala wa Rais Joe Biden.
Davinia alisema Waafghanistan hao watakuwa nchini Uganda kwa muda wa miezi mitatu kabla ya serikali ya Marekani kuwahamishia kwingineko.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja ni lini wataanza kuwasili.
Albania na Kosovo pia zimekubali ombi la Mareani la kuwapokea kwa muda, wakimbizi wa Afghanistan.