Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:45

Serikali ya Uganda yayafungia mashirika 54 yasiyo ya kiserikali


Rais Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni

Serikali ya Uganda ilisema Ijumaa imeamuru mashirika 54 yasiyo ya kiserikali kusitisha shughuli zake, ikiwa ni ongezeko kubwa katika juhudi za kudhibiti asasi za kiraia.

Makundi yaliyoathiriwa ni pamoja na shirika mashuhuri la haki nchini humo, Chapter Four, pamoja na makundi ya kidini, mazingira na demokrasia ya uchaguzi.

Kufungwa kwa shughuli hizo kuliamriwa kuanza mara moja, shirika la kitaifa kwa ajili ya NGOs, ambalo ni sehemu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema katika taarifa yake.

Ilisema kuwa vikundi vimeshindwa kuheshimu sheria inayohusu shughuli zao, pamoja na kufanya kazi wakati vibali vyao vimeisha muda, kutowasilisha mahesabu au kutosajiliwa na mamlaka.

Baadhi ya mashirika yaliyoamriwa kufunga shughuli zao yalishiriki katika operesheni ya ufuatiliaji wa uchaguzi siku ya kupiga kura, hapo Januari ambayo yalivamiwa na vikosi vya usalama, na wakati ambapo viongozi wao kadhaa walikamatwa.

Upigaji kura huo uliyokuwa na utata, ulishuhudia Rais Yoweri Museveni akirudi madarakani kwa muhula wa sita baada ya kampeni zenye ghasia zilizokuwa na unyanyasaji na kukamatwa kwa viongozi wa upinzani, kushambuliwa kwa vyombo vya habari pamoja na darzeni ya vifo vya watu.

XS
SM
MD
LG