Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:12

Uganda yaondoa baadhi ya masharti ya covid 19


Nesi akimdunga chanjo ya Astrazeneca mwanamke mmoja katika kituo cha afya cha Butanda April 27, 2021.
Nesi akimdunga chanjo ya Astrazeneca mwanamke mmoja katika kituo cha afya cha Butanda April 27, 2021.

Uganda imeondoa baadhi ya masharti ya Covid 19 baada ya siku 42, wakati mengine bado yakiendelea kutekelezwa.

Uganda imeondoa baadhi ya masharti ya Covid 19 baada ya siku 42, wakati mengine bado yakiendelea kutekelezwa. Kufungwa kwa shule bado kutaendelea, serikali inasema, huku baadhi ya wafanyakazi muhimu wakiwemo wa afya, wana usalama, waalimu na wale walio na umri wa zaidi ya miaka 45 wanapatiwa chanjo.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni Ijumaa usiku alitangaza kuondoa baadhi ya masharti ya Covid 19 baada ya takriban siku 42.

Museveni anasema uamuzi huo ulifanywa na kikosi kazi cha taifa baada ya kuona kuwa kesi zimepungua, na viwango vya watu kulazwa hospitali navyo pia vikiwa chini.

Miongoni mwa vigezo vingine, kikosi kazi pia kinafikiria kiwango cha utekelezaji hatua za usalama, taratibu ambazo zitafuatwa na umma na athari za kuendelea na kufungwa kwa shughuli kwa uchumi na wakazi kwa jumla. Hata hivyo bado kuna masharti ambayo yataendelezwa baada ya kuondolewa kwa baadhi.

“Muda wa kutotoka nje utabakia ule ule kuanzia saa moja usiku. Pili, boda boda hivi sasa zitaruhusiwa kufanya kazi mpaka saa 12 jioni. Wanaruhusiwa kubeba abiria mmoja. Shule zitaendelea kufungwa mpaka watu wengi wanaostahili kupatiwa chanja kati ya miaka 12 mpaka 19 watakuwa wamepata chanjo,” Rais Museveni amesema.

Vituo vya biashara hivi sasa vinahitajika kusafisha maeneo kwa ajili ya vibanda vya muda vya biashara na sehemu za ibada zitaendelea kufungwa kwa siku nyingine 60. Kwa kuongezea, matukio ya michezo yanayofanyika nje yatafanyika bila ya kuwepo watazamaji, baa na michezo ya ndani itaendelea kufungwa mpaka idadi inayostahili ya watu wawe wamepatiwa chanjo.

Huku baadh ya masharti yakiwa yameondolewa, Museveni anasema Mamlaka ya Taifa ya Mipango na maafisa wa kikosi kazi wataangalia kesi za Covid kama zitaweza kupungua mpaka 85 kwa siku ifikapo wiki ya tatu na kesi 66 kwa siku ifikapo siku ya 28. Maafisa wanawasihi raia kuheshimu taratibu za usalama ili kkuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.

Mpaka Julai 29, Uganda imeandikisha kesi mpya 252 na vifo 29 katika muda wa saa 48 za awali. Jumla ya kesi zilizothibitishwa ni 93,927.

Usafiri wa umma umeruhusiwa kuanza tena huku nusu ya idadi ya abiria wa kawaida wanaruhusiwa ndani ya mabasi na wakati magari binafsi yanaruhusiwa kuwa na watu watatu tu.

Waziri wa Afya wa Uganda, Jane Ruth Aceng anasema program ya kutoa chanjo ya Covid 19 kwa umma imepungua kasi kwasababu ya uhala wa chanjo kwasababu mahitaji yamevuka kiwango cha uzalishaji.

Aceng anasema serikali ya Uganda imetoa orodha ya chanjo ambazo zinaweza kutumiw anchini ikiwemo AstraZeneca, Johnson and Johnson, Pfirzer-BoioNtech, Sinopharm, Sinovac, Sputnik V, Sputnik Ligth na Moderna, akiongezea kwamba maafisa wa wizara ya afya wanafanya kila linalowezekana kupata chanjo.

Waziri Ruth Aceng anasema “mkakati wa serikali ya Uganda ni kuwapatia chanjo watu wengi katika taifa lenye takriban watu milioni 22, ambayo itawakilisha asilimia 48.8 kama njia muafaka ya kudhibiti janga na kufungua uchumi wa nchi. Kwa kuongezea, watoto wenye umri wa miaka 12 mpaka 15 watafikiriwa ili kuwakinga na virusi.”

Katika hotuba yake, Museveni amesema shule zitaendelea kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao, kitu ambacho kimezifanya shule nyingi na wanafunzi maskini kushindwa kumudu.

Ismail Kisule, mwalimu wa shule moja binafsi anasema mwaka uliopita ulikuwa mgumu sana kwa vile mapato yalikuwa hakuna.

“Tangu kufungwa mara ya kwanza, hatukupewa matumaini yoytote ya kurejea shule kufundisha. Hiyo ina maana hatulipwi. Kwahiyo, serikali inaposema watasubiri mpaka watu wengi zaidi wapatiwe chanjo ili tuweze kuanza kazi, hali yetu itazidi kuw ambaya na kutulazimisha kuacha kufundisha,” anasema Kisule.

Uganda imekamilisha mahitajiya kisheria ya kupata chanjo takriban dozi milioni 9 za AstraZeneca kupitia mpango wa COVAX. Kwa kuongezea, imeagiza dozi milioni mbili za Johnson and Johnson kutoka Umoja wa Afrika na imefanya malipo ya awali ya dola milioni 3.

Uganda mpaka sasa imepokea dozi 1,752,280 hivi karibuni kutoka China na Norway. Bado haiko bayana lini chanjo hizo zitasambazwa.

XS
SM
MD
LG