Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:34

Raia wa Afghanistan wawasili Uganda, wapatiwa hifadhi ya muda


Raia wa Afghanistan walioondolewa Kabuli wamewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe Uganda, August 25, 2021. REUTERS/Abubaker Lubowa
Raia wa Afghanistan walioondolewa Kabuli wamewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe Uganda, August 25, 2021. REUTERS/Abubaker Lubowa

Ndege iliyobeba watu waliohamishwa Afghanistan baada ya Taliban kuchukua udhibiti imeingia Uganda leo, ambako watapatiwa hifadhi ya muda , maafisa wamesema.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda imesema ndege iliyobeba raia wa Afghanistan 51 ikiwemo wanaume, wanawake na watoto ilitua katika mji wa Entebbe, ambako walipelekwa katika hoteli kwa msafara wa mabasi.

Raia wengine wa Afghanistan waliyohamishwa wanatarajiwa kuwasili Uganda hapo baadae wakitokea katika nchi hiyo iliyokumbwa na vita,

Wizara hiyo imeongezea, ikisema hatua hii inafuatia ombi la Marekani kuwapatia hifadhi ya muda raia hao wa Afghanistan na wengine walioko njiani kuelekea Marekani na maeneo mengine duniani.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa VOA Peter Clottey mapema wiki hii , Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Abubaker Odongo Jeje amesema nchi hiyo inayo uwezo wa kuwapokea.

“Tunao uwezo, tunalo eneo, tunayo ardhi, kwa kiwango chochote kama nilivyosema, bado tuko katika majadiliano. Tutajadiliana kuhusu wajibu wetu, majukumu yetu na nini wajibu na majukumu ya washirika wetu katika operesheni hii. Kwa hiyo haitakuwa ni kitu cha uganda peke yake, ” ameeleza Waziri.

Uganda inahifadhi wakimbizi wengi duniani karibu milioni 1.5 hiyo ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa wengi wakitokea Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

XS
SM
MD
LG