Jumatano, Rais wa Marekani na makamu wake Kamala Harris walifahamishwa kuhusu hali halisi nchini Afghanistan, wakati wakiwa kwenye ikulu.
Miongoni mwa masuala yaliozungumziwa ni pamoja na utoaji wa vibali maalum vya kusafiria kwa wahamiaji, maarufu SIV, pamoja na kuhakikisha usafiri salama kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Karzai mjini Kabul .
Taarifa tofauti zimeongeza kuwa Biden pia alizungumza na chancela wa Ujerumani Angela Merkel kuhusu haja ya kushirikiana katika kupeleka misaada ya kibinadamu kwa watu wa Afghanistan pamoja na kwenye mataifa jirani.
Ikulu ya Marekani imesema kuwa Marekani, Ujerumani na Uingereza wamekubaliana kufanya kikao cha kimitandao cha viongozi wa nchi saba tajiri Zaidi duniani, G7 wiki ijayo, ili kujadili hali nchini Afghanistan.