Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:32

Mataifa zaidi yaokoa raiya wake kutoka Afghanistan


Raiya wa Ufaransa wapanga foleni kuingia ndege ya kijeshi mjini Kabul
Raiya wa Ufaransa wapanga foleni kuingia ndege ya kijeshi mjini Kabul

Washirika wa Marekani kutoka muungano wa NATO, wanaendelea na juhudi za kuokoa raia wao kutoka Afghanistan, wakati vikosi vya mwisho vya Marekani vikiendelea kuondoka nchini humo siku chache tu baada ya kuanguka kwa serikali ya Rais Ashraf Ghani. 

Maafisa kadhaa wa Ulaya wameelezea wasi wasi wao kwamba hatua ya kuchukuliwa kwa serikali hiyo na Taliban huenda ikaongeza ugaidi pamoja na wimbi kubwa la wakimbizi barani humo.

Uingereza na washirika wengine wa NATO walianza kuondoa raia wao kutoka nchini humo Jumapili, wakiandamana na mamia ya raia wa Afghanistan waliofanya kazi pamoja.

Mataifa mengine ambayo yanaendelea kuondoa raia wao ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani, Uhispania na Italia, baada ya Marekani kuchukua tena udhibiti wa uwanja wa ndege wa mji mkuu wa Kabul ulioshuhudia ghasia mwishoni mwa wiki.

Mataifa mengi ya Ulaya yanatarajiwa kutangaza programu zao za dharura ili kutoa hifadhi kwa raia wa Afghanistan walioko kwenye hatari kutokana na kushirikiana nao katika miongo miwili iliyopita.

XS
SM
MD
LG