Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:27

Maelfu wasubiri kwa hamu ahadi ya Biden ya kuwaondoa nchini Afghanistan


Watoto wakifurahi na mwanajeshi wa Marekani wakiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai, Kabul, Afghanistan, Ijumaa Agosti 20, 2021, wakisubiri mchakato wa kuondolewa nchini kukamilika (Sgt. Samuel Ruiz/U.S. Marine Corps via AP)
Watoto wakifurahi na mwanajeshi wa Marekani wakiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Hamid Karzai, Kabul, Afghanistan, Ijumaa Agosti 20, 2021, wakisubiri mchakato wa kuondolewa nchini kukamilika (Sgt. Samuel Ruiz/U.S. Marine Corps via AP)

Maelfu ya watu nchini Afghanistan Jumamosi wanasubiri kwa hamu kubwa kuona ahadi ya Marekani iliyotolewa na Rais Joe Biden wiki hii ya kuwahamisha Wamarekani wote na wa Afghanistan waliosaidia katika juhudi ya vita kama itatekelezwa.

Wakati huohuo kiongozi wa Taliban amewasili Kabul kwa ajili ya mazungumzo na kundi la viongozi kwa ajili ya kuunda serikali mpya.

Kwa mujibu wa shirika la Habari la AP muda unakwisha kuendana na mpango wa Biden kwamba kufikia Agosti 31 iwe mwisho wa kuwaondoa wanajeshi wa Marekani waliobaki Afghanistan, na siku ya ijumaa rais hakusema muda utaongezwa.

Hata hivyo anakabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusu uamuzi wake juu ya kuondoka Afghhanistan wakati bado kuna ghasia za mara kwa mara nje ya uwanja wa ndege huku raia wa nchi hiyo wakikabiliwa na wasiwasi mkubwa wa kuwepo mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kundi la Taliban.

Katika maonyo mapya ya kiusalama, ubalozi wa Marekani Jumamosi uliwataka raia kutokwenda uwanja wa ndege wa Kabul bila kuwa na maelekezo binafsi kutoka kwa mwakilishi wa serikali ya Marekani, ukigusia kuwepo vitisho nje ya lango lake.

XS
SM
MD
LG