Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:48

Kuondoka Rais Ghani na uongozi wake kwatoa fursa kwa Wataliban


Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani na uongozi wake.
Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani na uongozi wake.

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani, pamoja na makamu wake na maafisa wengine wa waandamizi wameondoka nchini Jumapili, hatua iliyopelekea waasi wa Taliban kuchukua madaraka Afghanistan miaka 20 baada ya majeshi yaliyoongozwa na Marekani kuvamia na kuowaondoa madarakani.

Wajumbe wa ngazi ya juu wa tume ya kijeshi ya Taliban waliwasili katika makazi ya rais mjini Kabul wakati wapiganaji wa Taliban wakichukua udhibiti wa vituo muhimu vya mjini humo.

Msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amethibitisha Jumapili jioni kuwa wapiganaji walikuwa wamaelekezwa kulinda vituo vyote vya ulinzi na vituo vingine mjini Kabul ili “kuepusha vurugu na wizi baada ya majeshi ya Afghanistan kuvikimbia vituo vyao.”

Mujahid aliwasihi wakazi kuwa watulivu, akisema hatua hiyo ilikuwa inakusudia kuhakikisha usalama wa raia.

Hakuna maoni kutoka kwa Ghani wakati akiondoka Kabul. Katika ujumbe wa sauti uliorekodiwa Jumamosi, aliliambia taifa alikuwa anashauriana na wahusika ndani ya nchi na nje ya nchi juu ya hali ilivyo hivi sasa akiita ni “vita vya kulazimishwa.”

Abdullah Abdullah, mkuu wa Baraza la Usuluhishi la Taifa la Afghanistan, alibandika kanda ya video katika mtandao wa Facebook, akimkosoa Ghani.

Abdullah alithibitisha kuwa Ghani ameondoka Afghanistan na alisema, “Nahisi rais wa zamani aliondoka nchini na watu wako katika hali mbaya. Mungu ndiye atakaye mwajibisha.” Haijulikani mahali alipo Ghani.

Makamu wa Rais wa Afghanistan Amrullah Saleh, ambaye anasemekana alifuatana na Ghani na wengine walioondoka naye , katika ujumbe wa tweet aliahidi kutojisalimisha kwa Taliban, lakini hakujibu katika ujumbe wake taarifa za yeye kuondoka kwake nchini.

Katika ujumbe wa tweet, Waziri wa Ulinzi Bismillah Mohammadi amesema wao “wametufunga mikono nyuma ya migongo yetu na kuiuza nchi yetu, uovu wa mtu tajiri na genge lake,” akielekeza tuhuma hizo kwa Ghani na washirika wake.

XS
SM
MD
LG