Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:59

Canada kuwapa hifadhi wakimbizi 20,000 wa Afghanistan

Raia wa Afghanistan waliolazimika kukimbia makazi yao kutoka mikoa ya kaskazini, kufuatia mapigano kati ya wapiganaji waTaliban na vikosi vya usalama vya Afghanistan wakijihifadhi katika eneo la mapumziko Kabul, Ijumaa, Agosti. 13, 2021.

Canada ilisema Ijumaa itachukua hadi wakimbizi 20,000 wa Afghanistan wakiwemo viongozi wanawake, wafanyakazi wa serikali na wengine wanaokabiliwa na vitisho kutoka kwa Taliban.

Hatua hii iliyotangazwa na Canada imekuja wakati waasi wakionekana kusonga mbele nchini kote wakiteka miji mikubwa.

Hali nchini Afghanistan ni ya kusikitisha na Canada, haitakaa tu, Waziri anayehusika na masuala ya uhamiaji, Marco Mendicino aliuambia mkutano wa waandishi wa Habari.

Wakimbizi hao watajumuisha raia wa Afghanistan walio katika mazingira hatarishi ambao bado wako nchini humo au ambao tayari wamekimbilia mataifa Jirani.

Wakimbizi hao ni pamoja na viongozi wa kike na wafanyakazi wa serikali, pia inajumuisha watetezi wa haki za binadamu, watu wachache walioteswa na waandishi wa Habari.

Ndege kadhaa za wanaotafuta hifadhi zimeondoka na ndege ya kwanza ilitua Ijumaa huko Toronto, Mendicino alisema.

XS
SM
MD
LG