Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 19:44

Wataliban wakamilisha kuteka miji mitano mikuu Afghanistan


Ramani ya Afghanistan inaonyesha maeneo yaliyotekwa na Taliban mnamo mwezi Aprili 2021
Ramani ya Afghanistan inaonyesha maeneo yaliyotekwa na Taliban mnamo mwezi Aprili 2021

Taliban wamesema Ijumaa mashambulizi yao ya usiku yaliteka kabisa miji mikuu mitano ya majimbo nchini Afghanistan.

Miji hiyo ni pamoja na Kandahar kusini, Herat magharibi, Qahar-e-Naw upande wa kaskazini mashariki, Lashkar Gah uliopo upande wa kusini na mji muhimu wa Ghazni uliopo kusini mashariki.

Kuanguka kwa miji mikubwa kumeiwezesha Taliban kusonga mbele kuzunguka katika miji mkuu ya majimbo madogo, ikiwa ni pamoja na Tarinkot, mji mkuu wa jimbo la kusini la Uruzgan, Firuzkoh, mji mkuu wa Ghor ya kati, na Pol-e-Alam, mji mkuu wa jimbo la mashariki la Logar ambao ni mji anaotoka Rais Ashraf Ghani.

Taliban kupitia taarifa rasmi wamedai kuteka miji hii mpya na serikali ya Kabul haijapinga madai haya. Kwa hakika, gavana wa Uruzgan alitoa taarifa ya video akisema wazee wa kikabila na viongozi wa kisiasa walimuomba asiwazuie Taliban ili kuepusha umwagaji damu, kwa hivyo alikabidhi udhibiti kwa Taliban.

Taliban walithibitisha Ijumaa kuwa wamemkamata gavana wa zamani wa Herat, mbabe wa vita Ismail Khan, pamoja na wasaidizi wake kadhaa wa juu.

XS
SM
MD
LG