Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:34

Marekani yaipa Afghanistan dola milioni 100 kwa ajili ya wakimbizi


Rais Joe Biden
Rais Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden Ijumaa ameidhinisha dola milioni 100 za dharura kwa ajili ya mahitaji ya haraka ya wakimbizi nchini Afghanistan.

Biden pia ameidhinisha kutolewa dola milioni 200 katika huduma na mashirika ya serikali ya Marekani kukidhi mahitaji, ikulu imesema.

Marekani imejiandaa kuanza kuwahamisha maelfu ya wanaomba visa maalumu za uhamiaji kutoka Afghanistan ambao wanahatari ya kulipiziwa kisasi na waasi wa Taliban kwa sababu waliifanyia kazi serikali ya Marekani.

Kundi la kwanza la waliohamishwa na familia zao linatarajiwa kusafirishwa kabla ya mwisho wa mwezi kwenda Forty Lee kituo cha jeshi la Marekani kilichopo Virginia ambapo watasubiri utaratibu wa mwisho wa maombi ya visa zao.

Karibu raia 2500 wa Afghanistan wanatarajiwa kupelekwa kwenye kituo hicho kilichopo kusini mwa Richmond , Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema Jumatatu.

Utawala wa Biden unakagua vituo vingine ambapo waombaji wa visa wanaweza kupelekwa pamoja na familia zao.

Visa maalumu zinatolewa kwa wahamiaji wa Afghanistan waliofanya kazi kama wakalimani au katika kazi nyingine kwenye serikali ya Marekani wakati ilipoongoza uvamizi wa kijeshi mwaka 2001.

Chanzo cha Habari Reuters

XS
SM
MD
LG