Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 13:30

NATO kuendelea kuisaidia Afghanistan kimaendeleo na Kiusalama


Jens Stoltenberg
Jens Stoltenberg

Ushirika wa kijeshi wa nchi za Magharibi, NATO, utaendelea kuisaidia Afghanistan katika masuala ya maendeleo na kiusalama baada ya kuwaondoa wanajeshi wake kabla ya mwishoni mwa mwaka 2021.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amezungumza baada ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa ushirika huo mjini Brussels uliokuwa unatayarisha mkutano wa viongozi utakaohudhuriwa kwa mara ya kwanza na Rais Joe Biden.

Mkutano huo unalengo la kuimarisha tena umoja wao baada ya miaka minne ya misukosuko na utawala wa Donald Trump.

Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

Akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano wa mawaziri uliofanyika Jumanne, Jens Stolenburg anasema mawaziri walijadili juu ya agenda muhimu inayotayarishwa kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa June 14 mjini Brussels.

Mkutano huo utathibitisha tena umoja wa usshirika huo wa mataifa 30 na kutoa nafasi ya kihistoria kuanza ukurasa mpya wa ushirikiano.

Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa NATO ameeleza : "Mawaziri walizungumzia masuala mengi ikiwa ni pamoja na Afghanistan, Belarus, Rashia, China, na mahitaji ya NATO kwa ujumla ili kuweza kujitayarisha kwa ajili ya enzi mpya ya mashindano ya kila aina yanayo ongezeka duniani."

Kuhusiana na Afghanista, Katibu Mkuu wa NATO amesema mipango ya kuwaondoa wanajeshi inaendelea vyema kama ilivyopangwa na kwa usalama.

Stoltenberg ameongeza kuwa : "Tutaendelea na juhudi zetu za kidiplomasia mjini Kabul tukitoa ushauri na kutoa mafunzo ya kuziwezesha na kusaidia taasisi za kijeshi na usalama za Afghanistan. Tutazingatia pia juu ya operesheni maalum za kijeshi na kufanya kazi kugharimia huduza za kuwasaidia washirika wetu na jumuia ya kimataifa kuendelea kubaki Kabul na kutoa msaada."

Mawaziri walijadili pia juu ya kupanuka kwa ushawishi wa China duniani na athari za mabadiliko ya hali ya hewa masuala mawili muhimu kwa utawala wa Biden, pamoja na masuala ya ulinzi dhidi ya mashambuklio ya makombora, usalama wa mitandao na kupambana na kueneza habari za uongo.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden


Mawaziri walikuwa wanakutana kujadili pia suala la hali ya kisiasa nchini Belarus, rais wa taifa hilo Alexander Lukashenko alikuwa anazungumza na maafisa wa serikali akisema wanajeshi wa Rashia wako tayari kupelekwa nchini humo pindi kutakuwepo na kitisho kutoka NATO.

Alexander Lukashenko Rais wa Belarus amesema : "Hakujakuwepo na mazungumzo yeyote kuhusu kuletwa kwa wanajeshi wa Rashia au kuundwa kwa kambi ya kijeshi hapa Belarus. Suala hilo halikutajwa hata kidogo."

Hayo yote yakifanyika milipuko mitatu ilitokea kabul Jumanne jioni. Milipuko miwili ilikuwa mabomu yaliyolipuka katika maeneo mawili tofauti katika mitaa ya magharibi ya mji mkuu na kusababisha vifo vya watu 6 na saba kujeruhiwa kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan. Na mlipuko wa tatu uliharibu kituo cha umeme kaskazini mwa Kabul.

Waatalamu wanasema jeshi la Afghanistan ambalo linalotarajiwa kuwa na nguvu zaidi kuliko wapiganaji taliban ambao wameongeza mashambulizi yao mnamo mieizi ya hivi karibuni, limegubikwa na ulaji rushwa, ukosefu wa nidhamu na kushindwa kuchukua udhibiti wa taifa zima.

XS
SM
MD
LG