Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 06:47

Darzeni ya wanafunzi wa madrasa watekwa nyara jimbo la Niger


Wanafunzi waliokuwa wametekwa wa Chuo cha Sayansi cha Kagara wakiwa katika ukumbi wa serikali baada ya kuachiwa huru na watekaji wao huko Minna, Jimbo la Niger, Nigeria, Februari 27, 2021. -(Foto: AFP)
Wanafunzi waliokuwa wametekwa wa Chuo cha Sayansi cha Kagara wakiwa katika ukumbi wa serikali baada ya kuachiwa huru na watekaji wao huko Minna, Jimbo la Niger, Nigeria, Februari 27, 2021. -(Foto: AFP)

Polisi na maafisa wa jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Niger wanasema, genge la watu wenye silaha limewateka nyara darzeni ya wanafunzi katika madrasa moja iliyoko jimbo hilo siku ya Jumapili.

Serikali ya Niger imeandika kwenye ujumbe wake wa Twitter kwamba karibu wanafunzi 200 walikuwa katika shule hiyo ya Kiislamu wakati shambulio lilipotokea.

Taarifa zaidi zimesema haifahamiki bado ni wanafunzi wangapi waliotekwa nyara.

Utekaji huo umefanyika baada ya wanafunzi 14 kutoka chuo kikuu kimoja kaskazini magharibi mwa Nigeria wakishikiliwa kwa siku 40 kuachiliwa huru.

Katika habari nyingine msemaji wa polisi wa jimbo la Niger amesema kwenye taarifa watu waliokuwa na bunduki wakiwa kwenye pikipiki walishambulia mji wa Tegina katika wilaya ya Rafi jimbo hilo hilo jana saa tisa za mchana.

Hata hivyo hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusiana na shambulizi hilo.

XS
SM
MD
LG