Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:16

Mwanafunzi aeleza mkasa wa kutekwa wanafunzi Nigeria na namna alivyonusurika


Kikundi cha wanafunzi wa shule wakisindikizwa na jeshi la Nigeria na maafisa baada ya kuachiwa na watekaji wao wiki iliyopita, huko Katsina, Nigeria.(AP Photo/Sunday Alamba)
Kikundi cha wanafunzi wa shule wakisindikizwa na jeshi la Nigeria na maafisa baada ya kuachiwa na watekaji wao wiki iliyopita, huko Katsina, Nigeria.(AP Photo/Sunday Alamba)

Wakiandamana huku wameelekezewa bunduki katika msitu kwenye jimbo la kaskazini la Katsina, Nigeria, Usama Aminu Mali alikuwa ana mashaka iwapo yeye na mamia ya wanafunzi wenzake waliotekwa watanusurika.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 amesema alimsikia mmoja wa watekaji wake akiongea na simu na kuuliza, “Bwana, tuwaachie au tuwauwe? Amri ilitolewa: Endeleeni kutembea. Aliutuliza moyo wake, Usama aliendelea kutembea na kumuomba Mungu.

Aliokolewa siku ya Jumapili asubuhi, saa kama 30 baada ya watu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki walipovamia shule ya sekondari ya serikali ya wavulana ya mchepuko wa masomo ya sayansi karibu na mji wa Kankara Ijumaa jioni, wakiwateka mamia ya wanafunzi na kuelekea nao katika msitu wa Zango/Paula.

Mamlaka ya Jimbo la Katsina iliripoti kuwa hadi Jumanne takriban wanafunzi 320 bado hawajulikani walipo, siku hiyo hiyo kikundi cha kiislam chenye msimamo mkali cha Boko Haram kilidai kuhusika na kutekwa kwa wanafunzi hao.

Gavana wa Katsina, Aminu Bello Masari, alisema wavulana 839 walikuwa wamesajiliwa katika shule hiyo, kwa mujibu wa mtandao wa habari wa Marekani ABC News. Haijafahamika ni wanafunzi wangapi walikuwa shule wakati wa uvamizi huo, na wangapi waliweza kuwakwepa watekaji hao.

Sala na afya mbaya vlichangia kwa Usama kutoroka, alieleza wakati akisimulia mkasa huo kwa idhaa ya VOA Hausa. Kwa sababu ya maradhi sugu, alibakia nyuma – na hilo lilimuokoa.

Baada ya watu wenye silaha kuingia shuleni hapo na kuwazingira wanafunzi, “tulitembea usiku kucha msituni,” Usama alisema. “…Wengi wetu walipoteza viatu wakati wa harakati za kuondoka shuleni hapo. Nilikuwa natembea bila ya viatu na nilikanyaga miba.”

Kikundi cha wanafunzi waliokuwa wameachiliwa Disemba. 18, 2020 wakiwa mji wa Katsina, Nigeria.
Kikundi cha wanafunzi waliokuwa wameachiliwa Disemba. 18, 2020 wakiwa mji wa Katsina, Nigeria.

Kuna wakati mmoja siku ya Jumamosi, Usama alisikia ndege ikiruka juu na watu hao wenye silaha waliamuru tusimame. Baada ya helikopta kupita, mwanafunzi mwenye umri mkubwa zaidi aliamrishwa kutuhesabu.

“Tulikuwa 520,” Usama alisema. Watu hao wenye silaha “walituuliza nani atatulisha sote 520. Walisema sisi tulikuwa ni mzigo zaidi kuliko wasichana wa Chibok” – wanafunzi zaidi ya 200 waliokuwa wametekwa na Boko Haram kutoka shule moja huko jimbo la Borno upande wa kaskazini mashariki mwa Nigeria mwaka 2014.

Wasichana wasiopungua 100 hawajulikani waliko hadi sasa katika utekaji uliofanyika huko Chibok. Harakati za kuwaokoa zilichochea kuanzisha hashtag #BringBackOurGirls (Warejesheni Mabinti Zetu).

Baadhi ya Wasichana wa shule huko Chibok waliokuwa wametekwa wakionekana katika eneo lisiloweza kutambuliwa Januari 18, 2018.
Baadhi ya Wasichana wa shule huko Chibok waliokuwa wametekwa wakionekana katika eneo lisiloweza kutambuliwa Januari 18, 2018.

Usama alieleza kuwa watu wenye silaha huko Katsina, wakiwa na hofu ya kuonekana, waliwagawa wanafunzi katika makundi. Yeye alikuwa ni miongoni mwa kundi la watu 50, wakiwa na watu wanne wenye silaha mbele yao na wengine wakitembea sambamba na wanafunzi. Walitembea kwa saa kadhaa, huku wanafunzi waliokuwa na umri mkubwa wakilazimishwa kuwabeba wale waliokuwa hawawezi kutembea.

Manyayaso na kuzuiliwa kulichangia ugumu katika safari yao. “Walikuwa wanatupiga wakati tukitembea,” Usama alieleza walichofanya watekaji wao.

“Kulikuwa hakuna chakula, kwa hiyo tulianza kuokota matunda na majani kutoka katika miti iliyokuwepo. Nilikuwa nimedhoofika sana na sikuweza kusimama, hivyo wanafunzi wengine waliniletea majani nile. Yalimfanya mtu apate kiu, na hakukuwa na maji ya kunywa,” Usama alisema.

Wanafunzi waliendelea kutembea usiku wa kuamkia Jumamosi. “Baada ya kutembea kwa muda mrefu, walituambia tupige magoti huku wakisubiri wanafunzi wengine watufikie,” Usama alielezea kwa mujibu wa kumbukumbu aliyokuwa nayo. Alibaini walikuwa karibu na kijiji.

“Niliamua kutafuta sehemu ya kulala kwa sababu nilikuwa na maumivu makali,” mifupa iliniuma, alisema. “Sikuweza kutembea zaidi ya hapo. NIlikuwa najisemea moyoni, ‘ninaweza kubahatika kuachwa nyuma na watekaji hawa.’ Nilianza kumuomba Mungu.”

Watu hao wenye silaha wakijaribu kukwepa kuonekana, walilisogeza kundi kwenye sehemu yenye giza – na hawakubaini kuwa Usama hayumo katika kundi.

Usama alisema kuwa baada ya wengine kuondoka, alipata nguvu za kutosha kwenda msikitini katika kijiji hicho. Wakati wa alfajiri, muumini mmoja aliwasili – na Usama akakohoa ilia pate kumuona. Baada ya sala, waliohudhuria ibada walimpatia nguo kufunika sare zake za shule, na wakamlipa mwenye pikipiki ampeleke Osama kwa wazazi wake.

Serikali kuu ya Nigeria ilianza zoezi la uokoaji Jumamosi. Msemaji wa gavana wa jimbo la Katsina, Abdu Labaran, Jumatatu ameiambia CNN kuwa wanafunzi wasiopungua 446 wameokolewa kutoka kwa watekaji hao na wameweza kuungana tena na familia zao.

XS
SM
MD
LG