Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:03

Shule zafungwa Nigeria kufuatisha mashambulizi ya Boko Haram


Majimbo manne kaskazini mwa Nigeria yamefunga shule zote kufuatia tukio la kutekwa nyara kwa mamia ya wanafunzi katika jimbo la Katsina.

Amri hiyo ya shule kufungwa imetolewa katika majimbo ya Kano, Kaduna, Zamfara na Jigawa.

Muungano wa waalimu nchini Nigeria pia umetishia kufanya mgomo kulalamikia ukosefu wa usalama nchini humo.

Muungano huo umesema kwamba wanafunzi na waalimu wanalengwa na makundi yenye silaha Pamoja na wateka nyara.

Mamia ya wanafunzi walitekwa nyara wiki iliyopita, katika shule ya sayansi inayopatikana Kankara.

Kundi la wapiganaji wa kiislamu la Boko Haram limedai kuhusika na utekaji nyara huo.

Serikali kuu ya Nigeria haijatoa ripoti yoyote kuhusu mazungumzo na waliohusika katika utekaji nyara huo, kwa lengo la kuwaachilia huru wanafunzi hao.

Zaidi ya wanafunzi wavulana 300 hawajulikani walipo hadi sasa baada ya watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kushambulia shule ya sekondari mjini Kankara, katika jimbo la Katsina, kaskazini magharibi mwa Nigeria.

XS
SM
MD
LG