Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 16:12

Bunge la Nigeria limeanza mchakato wa kuharamisha malipo ya fidia


Wazazi na ndugu wa wanafunzi wa chuo cha serikali cha Misitu wakiwa wamebeba mabango wakati wa maandamano mjini Abuja kudai kuachiwa kwa wanafmilia wao waliotekwa (Picha na Kola Sulaimon / AFP) Mei 4, 2021.
Wazazi na ndugu wa wanafunzi wa chuo cha serikali cha Misitu wakiwa wamebeba mabango wakati wa maandamano mjini Abuja kudai kuachiwa kwa wanafmilia wao waliotekwa (Picha na Kola Sulaimon / AFP) Mei 4, 2021.

Bunge la taifa la Nigeria limeanza mchakato mpya wa kuharamisha malipo ya fidia kwa kundi lolote ambalo linawateka nyara na kutowaachilia mpaka walipwe fidia.

Katika mjadala wa mswaada wa kufanya marekebisho ya sheria ya kupinga ugaidi, wabunge na maseneta walisema malipo ya fidia huwapa watekaji nyara nia yakuendelea na udhalimu wao.

Wabunge wa Nigeria wameanza hatua za kuharamisha malipo ya fIdia kwa majambazi wanaotenda uhalifu, mswaada mpya ambao umejadiliwa bungeni na kurejeshwa kwenye kamati ya Seneti ya mambo ya sheria kuupitia kabla ya kuidhinishwa na kupitishwa kuwa sharia.

Changamoto ya kumaliza tatizo la utekaji nyara nchini humo lilielezewa kuwa ni muhimu sana, Seneta Ezenwan Onyewuchi aliupendekeza mswaada huo kwasababu ya matukio ambayo watekaji nyara hudai malipo ya fidia hali ambayo inaelezea inaendeleza vitendo vya utekaji nyara na kuimarisha majambazi.

Seneta Adamu Ailero anasema licha ya malipo ya fidia kuwa kinyume cha sheria, mashirika ya usalama yanapswa kupewa tecknolojia ya kisasa kuwafuatilia na kuwatafuta majambazi iliiwe rahisi kuwakamata.

Seneta Bamidele Opeyemi anasema kwamba mbali na kulipa fedha, familia za waathriwa waliotekwa nyara wakati mwingine wana laziimika kutoa vitu vingine kama pikipiki au magari kama fidia kabla jamaa zao kuachiliwa huru.

Mwishoni mwa majadiliano ya musada huo, Senata Onyewuchi alipendekeza muda wa kifungo jela uwe miaka 15 kwa mtu yeyote atakae kutwa na hatia ya kulipa fidia kwa majambazi.

Katika majadiliano haikuelezewa nini familia ya waliotekwa nyara inapaswa kufanya mbali na maoni kwamba serekali inapaswa kutimiza jukumu lake lakulinda vyema usalama wa watu, maisha na mali kote nchini.

Kuna uwezekano kwamba kamati ya senati juu ya masuala ya sharia inaweza kujumuisha hiyo katika uchunguzi na uwasilishaji wa muswada huo kabla haujasahihishwa.

XS
SM
MD
LG