Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:02

Nigeria : Wasichana 300 waliotekwa bado watafutwa, wavulana waachiliwa


Majina ya wanafunzi wa kike waliotekwa nyara na Boko Haram yamewekwa kwenye madeski ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 5 tangu kutwekwa Aprili 14 2019.REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo
Majina ya wanafunzi wa kike waliotekwa nyara na Boko Haram yamewekwa kwenye madeski ikiwa ni kumbukumbu ya miaka 5 tangu kutwekwa Aprili 14 2019.REUTERS/Afolabi Sotunde/File Photo

Watu wenye silaha nchini Nigeria Jumamosi wamewaachia vijana wa kiume 27 waliokuwa wametekwa kutoka shuleni kwao wiki iliyopita katika jimbo la kaskazini la Niger, wakati vikosi vya usalama vikiendelea kuwatafuta zaidi ya wasichana wa shule 300 waliotekwa katika jimbo jirani.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa shule zimekuwa zinalengwa ili kuteka idadi kubwa kwa ajili ya kudai fidia kaskazini mwa Nigeria, vitendo ambavyo vinafanywa na makundi yenye silaha ambayo watekaji wengi wakiwa wamebeba silaha na kuendesha pikipiki.

Mnamo Februari 17, wanafunzi 27, na wafanyakazi watatu na wanafamilia wao 12 walitekwa na genge lenye silaha baada ya kuvamia shule ya sekondari ya serikali ya mchepuo huko wilaya ya Kagara katika jimbo la Niger, na walinzi wa shule kuelemewa. Mvulana mmoja aliuawa wakati wa shambulizi hilo.

Baada ya kuachiliwa vijana hao walionekana na shahidi wa Reuters wakitembea na walinzi wenye silaha wakipita kwenye Kijiji chenye vumbi, wengine wakijitahidi kusimama na kuomba maji.

Afisa mmoja wa serikali amesema vijana hao wakiume walikuwa na umri kati ya miaka 15-18.

“Wanafunzi, wafanyakazi na ndugu wa shule ya sayansi ya serikali ya Kagara waliotekwa wameachiliwa huru na wamepokelewa na serikali ya jimbo la Niger,” Gavana Abubakar Sani Bello amesema katika ujumbe wa tweet.

Kuachiwa kwa wanafunzi wa kiume kumetokea siku moja baada ya shule ya jimbo la Zamfara kuvamiwa na watu wenye silaha na kuwateka wasichana 317.

Mashambulizi ya karibuni yameongeza wasiwasi juu ya kuongezeka uvunjifu wa amani unaofanywa na magenge yenye silaha na waasi wa Kiislam.

Kikundi cha jihadi cha Boko Haram kimekuwa kikifanya utekaji upande wenye mzozo wa kaskazini mashariki wa Nigeria, kama ilivyo kwa tawi la kikundi cha Islamic State.

Hali ya ukosefu wa usalama imekuwa ni tatizo la kisiasa kwa upande wa Rais Muhammadu Buhari, jenerali mstaafu na mtawala wa kijeshi wa zamani ambaye amekabiliwa na ukosoaji katika miezi ya karibuni kufuatia mashambulizi maarufu ya magenge yanayo julikana katika eneo kama “majambazi”.

Buhari aliwabadilisha wakuu wa jeshi wake waliokuwa madarakani kwa muda mrefu mwezi huu katikati ya hali ya kuongezeka kwa ghasia nchini Nigeria.

Mwezi Disemba, watu wenye silaha walivamia shule moja huko kaskazini magharibi katika jimbo la Katsina na kuwateka takriban wavulana 350, ambao baadae waliokolewa na vikosi vya usalama.

XS
SM
MD
LG