Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:11

Ajali ya ndege Nigeria yaua watu saba


Ajali ya Ndege Nigeria.
Ajali ya Ndege Nigeria.

Watu saba wamefariki katika ajali ya ndege ya jeshi la anga ya Nigeria.

Ndege hiyo ndogo aina ya Beechcraft King Air 350 ilianguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Abuja, Jumapili asubuhi.

Kulingana na taarifa ya maafisa wa jeshi, ndege hiyo iliripoti hitilafu katika injini yake.

Taarifa ya serikali iliongeza kuwa ndege hiyo ilikuwa inaelekea Minna, kiasi cha kilometa 110 kaskazini magharibi mwa mji mkuu. Waokoaji wako katika eneo na kwa masikitiko taarifa hiyo imesema wote waliokuwa ndani ya ndege hiyo wamefariki.

Vyanzo vya habari nchini Nigeria vimeeleza kuwa tayari viongozi wameamuru uchunguzi kufanywa mara moja.

Vikosi vya kadhaa vya anga vimetoa wito kwa watu kusubiri matokeo ya uchunguzi

Ndege hiyo kabla ya kuanguka na kuwaka moto ilionekana ikizunguka katika eneo la ajali karibu na njia ya ndege uwanjani hapo, mashuhuda wa ajali walieleza.

Mashuhuda hao walisikia mlio mkubwa kabla ya ndege hiyo kulipuka na kushika moto.

Mtu mwengine aliyeona ajali hiyo ameliliambia shirika la habari la Reuters kuwa mazingira ya eneo la ajali yalikuwa na harufu kali ya moshi na kemikali kutokana na kuwaka moto ndege hiyo.

XS
SM
MD
LG