Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:53

Ghasia nchini Mali zasababisha vifo vya mamia ya watu


Ramani ya Afrika Kaskazini
Ramani ya Afrika Kaskazini

Ghasia za karibuni nchini Mali, Niger na Jamhuri ya Afrika ya kati zimesababisha vifo vya mamia ya watu katika wiki za karibuni.

Lakini mwakilishi wa Marekani katika eneo la Sahel anasema kuna matumaini katika eneo hilo la Afrika Magharibi, wakati mataifa kadhaa hivi karibuni yaliitisha uchaguzi wa amani, huku chaguzi zaidi zikitarajiwa kufanyika mwaka huu wa 2021.

Mwakilishi wa juu wa Marekani kwa Sahel barani Afrika amekiri kwamba zilijkuwa wiki chache zenye vurugu katika eneo kubwa la Sahel – eneo ambalo lina mataifa ya Afrika Magharibi ya Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger.

Eneo hilo limegubikwa na wimbi la ghasia zenye kusababisha mauaji kutoka kwa makundi yenye msimamo mkali, huku zaidi ya matukio ya ghasia 1,000 yamelifanyika katika nusu ya kwanza yam waka 2020, kwa mujibu wa ripoti kutoka Mradi wa Maeneo ya Mizozo ya Silaha na Takwimu za Matukio.

Hivi karibuni, huko magharibi mwa Niger, wenye msimamo mkali walishambulia vijiji vitatu mnamo Januari 2, na kuua zaidi ya raia 100. Peter Pham, mwakilishi maalum wa Marekani kwa Sahel, amelaani vikali mashambulizi na kuwataka wana habari Jumane, kuwaita watenda maovu ‘wahuni’ na wasio muogopa ‘mwenyenzi mungu.’

Lakini haraka aliongezea kuwa kuna sababu ya kuwa na matumaini, wakati Nigeria inaelekea katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais mwezi Februari.

“Tumewapongezaz watu wa Niger ambao wametumia haki yao ya kidmokrasia ya kupiga kura katiak uchaguzi wa rais na wabunge hapo Desemba 27 na kutazamia duru ya pili ya uchaguzi wa rais kufanyika kwa mafanikio hapo Februari 21. Chaguzi hizi zinafanyika ikiwa ni matumaini ya kipindi cha kihistoria cha Niger katika makabidhiano ya amani ya madaraka kutoka rais mmoja aliyechaguliwa kidemokrasia kwenda kwa mwingine,” amesema Pham.

Si ajali, Pham amewaambia wana habari, kwamba kutaja uchaguzi na ukosefu wa uthabiti kwa wakati mmoja. Hiyo ni kwasababu ana azma kwamba milipuko hii ya ghasia kote katika eneo wana sababu moja inayofanana.

“Kiini cha mzozo huu katika Sahel, kama vilivyorejea kusisitiza, ni moja ya uhalali wa serikali – iwe ni mtizamo wa raia au la kwamba serikali yao ni halali, ina wajibu, uwezo, na iko tayari kukidhi mahitaji. Hii inajumuisha kuhakikisha sheria na uwajibikaji kwa ukiukaji wa haki za binadamu na manyanyaso yaliyotendwa na majeshi ya usalama. Serikali za Sahel kutochukua hatua ambazo zinaonyesha dhahiri nia ya dhati, hakuna kiwango cha kujihusisha kimataifa huenda kikaleta mafanikio.”

Ndiyo maana, ameongezea, kuwa msaada mkubwa wa serikali ya Marekani kwa eneo hilo unatolewa katika njia ya afya, maendeleo, na misaada ya kibinadamu. Marekani imewekeza zaidi ya $1.5 katika sekta hizo kuanzia mwaka 2017 mpaka 2019. Katika kipindi hicho hicho, amesema, Marekani imetoa kiasi cha $ 467 milioni katika msaada wa usalama.

Ornella Moderan, mtafiti ambaye anaongoza program ya Sahel kwa ajili ya taasisi ya masuala ya usalama, anakiri umuhimu wa uhalali wa serikali. Ameielezea Mali, ambayo ilikumbwa na mapinduzi mwezi Agosti kwasaabu ya ukosefu wa imani katika serikali.

Lakini amesema, kwa hakika kujenga serikali halali, jamii ni vyema ziungane pamoja kwa hiari yao na kwa dhati kujumuisha wote katika majadiliano yanayojumuisha wote, aliiambia VOA kutoka Bamako, Mali.

“Hivi sasa, swali nadhani, ni kwa kiwango gani washirika kutoka nje kama Marekani kwa hakika wanaweza kusaidia katika hili na kulishughulikia? Kuna haja kwa umiliki wa kitaifa na kuna haja ya mjadala wa kweli, kati ya watawala na mtu wa kawaida. Kwa hakika kiini cha kweli mahali ambako tupo hivi sasa, ni muhimu kwamba wakati tunajaribu kuweka tena mjadala wa kitaifa, ni vyema kuhajkikisha kwamba kila mtu anajumuishwa, na njia hii ni kuhakikisha hakuna kundi la kikabila ambalo litatengwa, hakuna makundi ya kidini, hakuna makundi ya kijinsia yataachwa kando. Kwa hakika hili lina changamoto, lakini muhimu sana.”

Je hilo linatokea? Pengine, amesema Pham, akielezea ucahguzi wa karibuni wa rais nchini Ghana na Burkina Faso, ambako wagombea urais waliokuwa madarakani walichaguliwa tena.

Pham alikwenda katika sherehe zote mbili za kuapishwa kwa maraisa hao akiwa sehemu ya ujumbe wa rais. Katika chaguzi zote mbili, upinzani ulilalamika haukuwa wa haki ingawaje matokeo hata hivyo yaliidhinishwa, na marais wote wawili wameapa kufanya kazi na raia wote.

XS
SM
MD
LG