Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:55

Wasichana zaidi ya 100 wa Chibok hawajulikani walipo miaka 7 baadaye


Majina ya watoto wa kike wa shule ya Chibok waliotekwa na kundi la Boko haram huko Nigeria.
Majina ya watoto wa kike wa shule ya Chibok waliotekwa na kundi la Boko haram huko Nigeria.

Ofisi ya rais wa Nigeria imeapa kuwaokoa wasichana wa zamani wa shule 112 wanaosadikiwa kubaki katika mikono ya kundi la Boko Haram tangu walipotekwa nyara kutoka mji wa Chibok miaka saba iliyopita. Wakosoaji wanashutumu serikali kwa kutofanya vya kutosha kuokoa wasichana hao ambao sasa ni wanawake au kuboresha usalama wa shule.

Taarifa iliyopewa jina la “Wasichana wa Chibok Bado wako akilini mwetu” ilitolewa na ofisi ya rais Alhamisi wakati Nigeria inaadhimisha miaka saba tangu wasichana wa shule 276 kutekwa kutoka kwenye shule ya serikali huko Chibok, katika jimbo la Borno.

Mamlaka ilisisitiza wito wake wa kuwatafuta na kuwakomboa wasichana hao 112 waliobaki kifungoni.

Lakini wazazi na watetezi wanashutumu serikali kwa uzembe na kutoa ahadi hewa. Allen Manase ni mkuu wa vyombo vya habari na utangazaji wa jamii ya Chibok.

Karibu wasichana 503 walikuwa shuleni hapo usiku wa kutekwa nyara na Boko Haram mwezi Aprili 2014. kati ya 276 waliochukuliwa, zaidi ya 100 waliachiliwa kupitia mazungumzo, wakati wengine walifanikiwa kutoroka.

Wiki hii, katika kuadhimisha miaka saba tangu utekaji nyara wao, wazazi wa wasichana waliobaki walikusanyika shuleni kuombea kurudi kwao salama.

Manase anasema serikali iko kimya zaidi juu ya suala hili lakini inalenga tu katika maadhimisho hayo kutoa taarifa.

Katika miezi ya hivi karibuni, utekaji nyara kadhaa mkubwa wa wanafunzi umetokea kaskazini mwa Nigeria, na kusababisha kufungwa kwa shule.

Ripoti mpya ya Amnesty International ilisema zaidi ya shule 600 kaskazini mwa Nigeria zimefungwa kwa sababu ya ukosefu wa usalama tangu Desemba.

Nigeria ina idadi kubwa zaidi ya wanafunzi walioacha shule ulimwenguni kulingana na UNICEF, haswa kwa sababu ya ukosefu wa usalama kaskazini, ambapo uandikishaji wa shule na kiwango cha kusoma ni kidogo sana.

Wakati wazazi wengi wanaendelea kungojea na kutumaini, mawakili na Amnesty International wanasisitiza mamlaka kuzifanya shule ziwe salama.

XS
SM
MD
LG