Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 03:53

Watu angalau 55 waliuawa katika mashambulizi huko DRC


Vijiji vimechomwa moto na raia kutekwa katika mashambulizi hayo
Vijiji vimechomwa moto na raia kutekwa katika mashambulizi hayo

Jeshi na kundi la haki za kiraia katika eneo, liliwalaumu Allied Democratic Forces (ADF), kundi la kiislam lenye silaha, kwa kuvamia Kijiji cha Tchabi na kambi moja ya watu waliokoseshwa makazi karibu na kijiji kingine cha Boga. Vyote vipo karibu na mpaka wa Uganda

Watu angalau 55 waliuawa katika mashambulizi mawili ya usiku kucha kwenye vijiji huko mashariki mwa Congo, Umoja wa Mataifa ulisema Jumatatu katika usiku ambao ulikuwa mbaya sana kwenye eneo ambalo limeshuhudia ghasia katika kipindi cha takriban miaka minne.

Jeshi na kundi la haki za kiraia katika eneo, liliwalaumu Allied Democratic Forces (ADF), kundi la kiislam lenye silaha, kwa kuvamia Kijiji cha Tchabi na kambi moja ya watu waliokoseshwa makazi karibu na kijiji kingine cha Boga. Vyote vipo karibu na mpaka wa Uganda.

Nyumba zilichomwa moto na raia kutekwa, ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya haki za binadamu ilisema katika taarifa yake.

Albert Basegu, mkuu wa kundi la haki za kiraia huko Boga, aliliambia shirika la habari la Reuters kwa njia ya simu kwamba aliarifiwa juu ya shambulizi hilo kwa sauti za kilio kwenye nyumba za jirani. Anasema nilipofika huko, niligundua kuwa washambuliaji tayari walikuwa wamemuua mchungaji wa kianglikana wakati binti yake alijeruhiwa vibaya.

Kivu Security Tracker (KST) kitengo ambacho kinarekodi ghasia huko mashariki mwa Congo tangu mwaka 2017 kiliandika kwenye Twitter, mke wa mkuu katika eneo hilo alikuwa miongoni mwa waliokufa. Haikuelezea nani alihusika na mauaji hayo.

Ni siku mbaya kabisa kuwahi kurekodiwa na KST, alisema Pierre Boisselet, mratibu wa kundi la utafiti.

ADF inaaminika imeua zaidi ya watu 850 mwaka 2020, kulingana na Umoja wa Mataifa, katika kesi nyingi za mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa raia, baada ya jeshi nchini humo kuanza operesheni dhidi yake mwaka mmoja uliopita.

XS
SM
MD
LG