Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 08:02

Kiongozi wa kundi la Polisario arejea Algeria kutoka Spain


Kiongozi wa kundi la Polisario , Brahim Ghali
Kiongozi wa kundi la Polisario , Brahim Ghali

Ripoti zinasema kuwa kiongozi anayeongoza kundi linadai uhuru kutoka Morocco Brahim Ghali na aliezua mzozo wa kidiplomasia kati ya Rabat na Madrid baada ya kupelekwa kupata matibabu nchini Spain, amerejea Algeria usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Ghali alitolewa kwenye hospitali kaskazini mwa Spain, baada ya kupata matibabu kwa wiki sita kufuatia kuugua COVID-19 kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa shirika hilo la habari na taifa lake lililojitangazia uhuru wa Sahrawi lenye makao yake makuu kwenye kambi za wakimbizi magharibi mwa Algeria.

Ghali ndiye kiongozi wa eneo hilo pamoja na kundi la Polisario Front, ambalo kwa muda mrefu limejitahidi kujikwamua kutoka utawala wa Morocco iliyo jichukulia udhibiti wa Sahara Magharibi kwenye miaka ya 70 wakati likijitahidi kurejesha uhuru wake tangu wakati huo.

Ghali ameondoka Spain saa chache baada ya kutoa ushahidi Jumanne mbele ya wachunguzi kwa njia ya video kutokana na tuhuma za kuongoza mateso, mauwaji ya kimbari pamoja na ukatili mwingine. Jaji mmoja wa Spain alitoa uamuzi kuwa Ghali awe huru wakati uchunguzi ukiendelea.

XS
SM
MD
LG