Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:56

Waziri wa Uchukuzi wa Uganda ajeruhiwa, bintiye na dereva wauawa kwa kupigwa risasi


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Jenerali Katumba Wamala.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Jenerali Katumba Wamala.

Watu wenye silaha, Jumanne walishambulia kwa risasi, gari la waziri wa Ujenzi na uchukuzi wa Uganda, katika jaribio la kutaka kumuua, kwa mujibu wa mafisa wa serikali ya nchi hiyo.

Washambuliaji hao walimuua binti wa waziri huyo na dereva wake, msemaji wa jeshi na vyombo vya habari wamesema.

Waziri huyo ambaye ni kamanda wa zamani wa jeshi, alijeruhiwa.

Kituo cha Televisheni cha Uganda, NBS, kiliripoti kwamba washambuliaji wanne waliokua kwenye pikipiki walifyatua risasi, kwenye gari lililokuwa linambeba Jenerali Katumba Wamala. Shambulio hilo lilitokea katika kitongoji cha Kiasasi mjini Kampala.

“Kumefanyika shambulio la risasi lililomlenga yeye, amejeruhiwa na amepelekwa hospitali. Dereva wake aliuwawa,” msemaji wa jeshi Brigedia Flavia Byekwaso ameliambia shirika la habari la Reuters.

Mbunge Chris Baryomunsi amethibitishwa kwamba binti wa waziri Wamala, ambaye alikua naye ndani ya gari aliuwawa.

Miaka ya karibuni, kumekuwa na visa kadhaa vya mauaji, ambayo hayajafanyiwa uchunguzi wa kutosha, pamoja na vifo vya kushangaza ,vya maafisa mashuhuri katika nchi hiyo ya Afrika mashariki, ambayo yamechochea uvumi, juu ya wahusika na nia yao.

Miongoni mwa waliouwawa, ni mbunge, afisa wa polisi wa ngazi ya juu , muendesha mashtaka mkuu wa nchi, viongozi wa kiislamu na wengine. Karibu mauaji yote hayo yalitekelezwa na watu waliokua kwenye pikipiki.

-Imetayarishwa na Patrick Nduwimana

XS
SM
MD
LG