Mabadiliko hayo yanatokana na takwimu za hivi karibuni zinazoonesha kwamba kiwango cha uzazi kimeshuka sana katika taifa hilo lenye wakazi wengi zaidi duniani.
Bejing iliondoa sera ya miongo mingi ya mtoto mmoja kwa familia mwaka wa 2016, na kuruhusu kiwango cha watoto wawili, ikijaribu kuepusha matatizo ya kiuchumi yanayotokana na kuongezeka kwa haraka idadi ya wazee nchini humo.
Lakini mabadiliko hayo hayajafanikiwa kuleta matokeo endelevu katika uzazi kutokana na kupanda sana kwa gharama za kulea watoto nchini China, changamoto iliyopo hadi wa leo.