Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:05

Mzozo wa Misri na Ethiopia unazidi kuongezeka juu ya bwawa Renaissance


Eneo la bwawa Renassaince huko Ethiopia
Eneo la bwawa Renassaince huko Ethiopia

Vyombo vya habari vya Misri vilitangaza taarifa ya hasira iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ahmed Hafez akikosoa tangazo la Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwamba atajenga  mabwawa 100 mapya yenye ujazo mdogo na wa wastani

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje nchini Misri alipinga Jumanne baada ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kuashiria alikuwa anapanga kujenga mabwawa 100 yenye ujazo mdogo hadi wa wastani katika kipindi cha mwaka unaokuja. Bado hakuna suluhisho kwa mzozo unaoendelea kwenye bwawa la Renaissance kwenye mto Nile ndani ya eneo la Ethiopia.

Vyombo vya habari vya Misri vilitangaza taarifa ya hasira iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje Ahmed Hafez akikosoa tangazo la Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed kwamba atajenga mabwawa 100 mapya yenye ujazo mdogo na wastani kwenye njia za maji nchini mwake katika kipindi cha mwaka ujao.

Hafez aliashiria kwamba mpango huo ni dalili ya nia mbaya ya Ethiopia kuhusu mzozo juu ya kujaza bwawa la Renaissance ambalo limesababisha malumbano yasio ya kawaida na wote Misri na nchi jirani ya Sudan. Hafez aliongeza kuwa Ethiopia lazima iratibu mipango kama hiyo na majirani zake kabla ya kuwasababishia uharibifu.

Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sissi.
Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sissi.

Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sissi alitembelea Djibouti wiki iliyopita akisisitiza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, kwamba alikuwa bado ana matumaini ya mashauriano ya kidiplomasia, kusuluhisha mzozo na Ethiopia, juu ya kujaza bwawa.

Tulijadiliana hali ya bwawa la Renaissance, ambalo linaathiri maslahi ya eneo zima katika ukanda huu, na umuhimu wa makubaliano ya haki na yenye usawa juu ya kujaza maji na kuendesha bwawa hilo, haraka iwezekanavyo, na Misri kukataa juhudi za upande wowote kuweka mpango wake ambao haukidhi maslahi au haki za nchi ambazo maslahi yao yameathiriwa.

Mwanasosholojia wa kisiasa nchini Misri, Said Sadek ameiambia VOA suala la Ethiopia kujaza maji kwenye bwawa la Renaissance kwa mwaka wa pili kuanzia Julai, limechochea hasira za umma kwa wa Misri.

“Maoni ya umma ya ghadhabu sana, na yanaishinikiza serikali kujibu uchokozi wa wanasiasa wa Ethiopia na vyombo vya Habari, ambavyo kila wakati wanazungumza kwa njia ya uchochezi dhidi ya watu wa Misri na serikali ya Misri”

Sadek aliendelea kusema kwamba vikosi vya upinzani vya Misri, ambavyo vingi vipo nje ya nchi, vimekuwa vikiitisha maandamano, juu ya kile walichodai serikali kutosimamia vyema tatizo hilo.

Mawaziri wa Misri, Ethiopia na Sudan wakati wa mazungumzo juu ya bwawa Renaissance hapo April, 2021
Mawaziri wa Misri, Ethiopia na Sudan wakati wa mazungumzo juu ya bwawa Renaissance hapo April, 2021

Sadek aliongeza kuwa maafisa wa Misri, walishangaa juu ya kutokuwa tayari kwa ushawishi wenye nguvu, wa mataifa ya kigeni kama vile EU, Marekani na Umoja wa Afrika, kutumia ushawishi wao, kufikia suluhisho la kidiplomasia kwenye tatizo hili.

Paul Sullivan, profesa katika chuo kikuu cha ulinzi cha kitaifa cha Washington nchini Marekani, anaiambaia VOA kwamba ujenzi wa Ethiopia wa bwawa la Grand Renaissance (GERD) ni mtafaruku wa kutosha, lakini kujenga zaidi ya mabwawa 100, kunaleta uchochezi zaidi, na ni uchokozi, unaoongezeka.

Anaendelea kusisitiza kwamba Misri itahitajika kujibu, na ikiwa Ethiopia inataka amani, wanatoa ishara tofauti. Kama hali hii itakuja kuwa vita, anawasihi wote watashindwa, na kwa kiasi kikubwa. Anasema makazi ya kuafikiana itakuwa bora, lakini kwamba mambo, yanaonekana kwenda kinyume.

Jeshi la Misri limekuwa likifanya mbinu za kiufundi na nchi kadhaa za eneo katika siku za karibuni, pamoja na Sudan, kwa ajili ya kuonesha utayari wake katika tukio hilo, mara mzozo ukizuka.

XS
SM
MD
LG