Zoezi hilo la kukabidhi udhibiti limethibitishwa Ijumaa na afisa mmoja wa ulinzi wa Marekani kwa Sauti ya Amerika.
Kwa karibu miongo miwili kambi hiyo iliyo takriban kilomita 60 kaskazini mwa mji wa Kabul, ilikuwa kituo kikuu cha jeshi la Marekani katika vita vya kuondoa vikosi vya Taliban mamlakani, na kuwaua magaidi wa al-Qaida.
Al-Qaida wanaoshutumiwa kuua maelfu ya Wamarekani katika mashambulizi ya Septemba 11, 2001.
Msemaji wa wizara ya Ulinzi ya Afghanistan Ijumaa amethibitisha kuondolewa kwa wanajeshi wote wa kigeni kutoka Bagram.
Jenerali Austin "Scott" Miller, Kamanda wa majeshi ya Marekani nchini Afghanistan bado yuko nchini akisimamia vikosi vya Marekani vilivyosalia kulingana na afisa huyo.
Vyanzo vya habari : VOA Swahili / AP