Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 17:40

Trump na Biden washiriki katika maombolezi ya wahanga wa Septemba 11


Mgombea Urais wa chama cha Demokratik ambaye alikuwa Makamu wa Rais Joe Biden akisalimiana na Makamu wa Rais Mike Pence katika maadhimisho ya 19 ya shambulizi la kigaidi la Sept. 11 Katika eneo la kumbukumbu ya taifa ya Septemba 11, New York, on Ijumaa, Septemba 11, 2020.
Mgombea Urais wa chama cha Demokratik ambaye alikuwa Makamu wa Rais Joe Biden akisalimiana na Makamu wa Rais Mike Pence katika maadhimisho ya 19 ya shambulizi la kigaidi la Sept. 11 Katika eneo la kumbukumbu ya taifa ya Septemba 11, New York, on Ijumaa, Septemba 11, 2020.

Marekani inaadhimisha Ijumaa miaka 19 tangu mashambulizi mabaya kabisa ya kigaidi kwa kuhudhuria ibada ya kuwakumbuka watu 3,000 waliouawa mjini New York, Washington DC na Shanksville, Pennsylvania.

Wananchi, família za waathriwa na wanasiasa wamekusanyika katika miji hiyo mitatu kwa sherehe zinazofanyika kila mwaka tangu kutokea mashambulizi hayo kwa kusoma majina ya waliofariki.

Wagombea urais Donald Trump na Joe Biden wamehudhuria sherehe zilizofanyika Shanksville ambako ndege ya shirika la ndege la United 93 ilianguka. Katika sherehe hizo majina ya wale wote waliofariki hutajwa.

Mashambulio hayo ambayo kundi la Al-Qaida likiongozwa na Osama bin laden lilidai kutekeleza yalipelekea Marekani kuishambulia Afghanistan na kuuondoa madarakani utawala wa Taliban.

Mapigano hayo yanaendelea hadi hii leo ambapo kuna dalili za vita kumalizika kutokana na kuanza kwa mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Afghanistan na wapiganaji wa Taliban ya kisimamiwa na Marekani yatakayoanza siku ya Jumamosi.

Mike Pompeo
Mike Pompeo

Akiwa njiani kuelekea Doha Qatar siku ya Ijumaa kuhudhuria mazungumzo hayo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege yake ameyataja mazungumzo hayo kuwa ni ya kihistoria.

Pompeo amesema : "Tuna taraji hapo Jumamosi asubuhi kwa mara ya kwanza katika karibu miongo miwili sasa Waafghanistan watakaa pamoja kwenye meza moja kuweza kutayarisha kile kitakachokuwa mazungumzo yatakayoendelea juu ya namna ya kuendelea mbele na nchi yao na kupunguza mapigano na ghasia na kuleta upatanishi kati ya wa Afghanistan.

Kwa upande mwingine ripoti mpya iliyotolewa na chuo kikuu cha Brown hapa Marekani juu ya gharama za vita vinane ambavyo Marekani ilianzisha au kuhusiska tangu mashambulizi ya Septemba 11, 2001, vimesababisha karibu wakimbizi milioni 37 kote duniani.

Ripoti hiyo iliyochapishwa mapema wiki hii, inaeleza idadi hiyo ambayo huenda ikawa china ya idadi halisi imezidi idadi ya watu waliopoteza makazi yao kwa vita au majanga tangu mwanzo wa karne ya 20, ispokuwa tu idadi ya wakimbizi iliyotokea baada ya vita vya pili vya dunia.

Kulingana na ripoti hiyo wengi wa wakimbizi walolazimika kuhama makazi yao ni kutoka Afghanistan, Iraq, Pakistan, Yemen, Somalia, Libya na Syria.

Rais Donald Trump akizungumza katika maadhimisho ya Septemba 19, huko Shanksville, Pa., Ijumaa, Sept. 11, 2020. (AP Photo/Gene J. Puskar)
Rais Donald Trump akizungumza katika maadhimisho ya Septemba 19, huko Shanksville, Pa., Ijumaa, Sept. 11, 2020. (AP Photo/Gene J. Puskar)

Na katika lengo la kutekeleza ahadi zake za kampeni za kumaliza vita vinavyohusisha wanajeshi wa Marekani Rais Trump anatazamiwa kutangaza hivi karibuni juu ya kupunguza wanajeshi huko Afghanistan.

Mapema wiki hii kamanda mkuu wa makao makuu ya kijeshi kanda ya kati huko Ulaya na Mashariki ya kati Jenerali Frank Mckenzie alitangaza kupunguzwa wanajeshi wa Marekani nchini Irak mwezi Septemba kutoka elfu 5,200 hadi 3000 alipotembeea wanajeshi mjini Baghdad.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG