Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:41

Biden na Trump watofautiana jinsi ya kuendesha kampeni 


Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden (kushoro) na Rais wa Marekani Donald Trump
Makamu wa Rais wa zamani Joe Biden (kushoro) na Rais wa Marekani Donald Trump

Kampeni za uchaguzi zikingia awamu ya mwisho ya miezi mwili iliyobaki, rais Donald Trump na mpinzani wake Joe Biden wa chama cha Demokratik wote wanaimarisha safari zao kwenye majimbo yenye ushindani mkubwa wiki hii. 

Lakini wagombea hao wawili wanatofautiana kabisa katika mikakati ya kampeni zao na ujumbe kwa mashabiki wao. Trump ameanza kufanya mikutano mikubwa ya hadhara wakati Biden anakutana na makundi madogo madogo ya watu kutokana na janga la corona.

Rais Donald Trump anasafiri katika majimbo matano yenye ushindani wiki hii ya Florida, North Carolina, Michigan, Pensnsylvania na Nevada.

Ameanza tena mikutano yake ya hadhara akikusanya maelfu ya mashabiki, akisema hakuna tofauti na maandamano na mikusanyiko inayofanyika ya kupinga ubaguzi ya Black Lives Matter.

Donald Trump asema : “Ikiwa uko tayari kufanya ghasia na kukabiliana na wenzako uso kwa uso na kufanya chochote unachotaka kufanya, ukiwa unafanya hivyo kwa sababu inachukuliwa ni haki yako ya kuandamana kwa amani. Basi sisi tumeamua kuitisha mikutano ya hadhara kwa amani kulalamika pia.”

Polisi wakijaribu kudhibiti ghasia kati ya upande unaomuunga mkono Rais Donald Trump na waandamanaji wanaopaza sauti maisha ya mtu mweusi yanathamani nje ya jengo la Bunge la jimbo la Oregon huko Salem, Oregon, Marekani September 7, 2020.
Polisi wakijaribu kudhibiti ghasia kati ya upande unaomuunga mkono Rais Donald Trump na waandamanaji wanaopaza sauti maisha ya mtu mweusi yanathamani nje ya jengo la Bunge la jimbo la Oregon huko Salem, Oregon, Marekani September 7, 2020.

Kwa upande wake mgombea wa Demokratik Biden amekutana na wafuasi wake katika vikao vidogovidogo bila ya kukaribiana katika jimbo la Pennsylvania wiki hii.

Todd Belt, Profesa wa sayansi ya siasa katika chuo kikuu cha George Washington anasema kampeni ya Biden inategemea sana matukio kupitia mtandao, ikijaribu kumulika kwamba mgombea wao ni kiongozi mwenye hisia na huruma anaetaka kuepusha wananchi kuingia katika hali ya hatari.

Mgombea urais wa chama cha Demokratik Joe Biden akiwa katika kampeni huko eneo la Mill 19 in Pittsburgh, Pa., Jumatatu, Agosti. 31, 2020. (AP Photo/Carolyn Kaster)
Mgombea urais wa chama cha Demokratik Joe Biden akiwa katika kampeni huko eneo la Mill 19 in Pittsburgh, Pa., Jumatatu, Agosti. 31, 2020. (AP Photo/Carolyn Kaster)

Profesa huyo anaefafanua zaidi : Atakuwa katika mikusanyiko ya watu wachache na hivyo kuweza kusikiliza kile watu wanasema. Na hiyo ni sehemu ya kupigania haki za kijamii pamoja na haki za afya na uchumi katika ujumbe wake. Wakati rais Trump anataka mikusanyiko mikubwa ya watu. Anataka kuonesha kwamba ana ungaji mkono mkubwa kwa kile anachokieleza ni wengi wa marekani waliokimya, na yeye yuko katika kinyan’ganyiro hichi kuwakilisha wafuasi hao.”

Basi akiwa katika kampeni yake jana huko MichIgan Biden alimshambulia Trump kutokana na habari kwenye kitabu kitakachotolewa hivi karibuni cha mwandishi wa habari mashuhuri Bob Woodward kwamba rais alikiri hapo mwezi Februari kwamba hakulipatia umuhimu mkubwa janga la corona ili kuepusha taharuki.

Joe Biden anaeleza : "Alikuwa na habari zote, alifahamu jinsi ilivyo hatari. na wakati ugonjwa huu wa hatari ulipokuwa unasababisha maafa kote nchini , alishindwa kufanya kazi yake. Amewasaliti wananchi wa Marekani.

Rais Trump alijibu tuhuma hizo mara moja akisema : "Hatutaki kuwa na hali ya taharuki. Hatutasababisha taharuki. Na hicho ndicho nilichokifanya. Na nilieleza hayo bayana.”

Trump akiwa katika kampeni huko Michigan.
Trump akiwa katika kampeni huko Michigan.

Uchunguzi wa maoni unaonyesha kwamba wapiga kura wamehamasika kutokana na janga na kwamba Wamarekani wengi hawafurahishwi na jinsi Trump anavyo kabiliana na janga la corona, jambo ambalo kampeni ya Biden inahamu sana kumulika.

Lakini wakati Trump yuko nyuma katika maoni ya wapiga kura kote nchini anakaribiana sana na biden katika majimbo yenye ushindani.

Hapo Kesho wote Trump na Biden wamepanga kuadhimisha mashambulio ya septemba 11 huko Shanksville Pennsylvania eneo la ajali moja kati ya ndege tatu zilizotekwa nyara na magaidi siku hiyo.

XS
SM
MD
LG