Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 20:27

Trump kupunguza misaada kwenye miji itakayofinya fedha kwa idara za Polisi


Rais Trump akihutubia wafuasi wake.
Rais Trump akihutubia wafuasi wake.

Ni muhimu kwa serikali kuu  ipitie upya matumizi ya fedha zake  kwa maeneo  ambayo yanaruhusu machafuko-Trump

Rais wa Marekani Donald Trump ameanza mzozo mpya kwa miji inayoongozwa na wademokrat akiwaamuru maafisa wa juu kuangalia ikiwa kama serikali ya kitaifa inaweza kupunguza msaada wa serikali kuu kwenye manispaa.


Katika barua ya Jumatano, Trump aliielekeza Ofisi ya Usimamizi na Bajeti ya Ikulu kutoa mwongozo kwa idara za serikali kuu kukata ufadhili kwa miji ambayo itapunguza fedha kwa idara zao za polisi baada ya wiki kadhaa za maandamano ya mijini kumlenga Trump na manyanyaso ya polisi kwa watu walio wachache.


"Utawala wangu hautaruhusu dola za serikali kuu kufadhili miji ambayo inawaruhusu kuzorota katika maeneo yasiyofuata sheria," ujumbe wa rais ulisema. Ni muhimu kwa serikali kuu ipitie upya matumizi ya fedha zake kwa maeneo ambayo yanaruhusu machafuko, vurugu, na uharibifu katika miji ya Amerika.

Jaribio lolote la kukata misaada hiyo linaweza kupata changamoto ya kisheria kutoka kwenye miji iliyoathiriwa. Baraza la Congress linapitisha ufadhili huo, lakini maafisa wa utawala wanaweza kujaribu kuzuia miradi fulani.

XS
SM
MD
LG