Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 07:44

Maafisa wa serikali Marekani wanaielezea sheria ya Hatch na matumizi White House


Mandhari ya bustani ya Rose Garden iliyokarabatiwa katika eneo la White House.
Mandhari ya bustani ya Rose Garden iliyokarabatiwa katika eneo la White House.

Melania Trump, mke wa Rais Trump anatumia bustani ya Rose Garden iliyofanyiwa  ukarabati katika viwanja vya White House kama mahala anapotolea hotuba yake ya Jumanne ya moja kwa moja kwenye mkutano mkuu wa chama cha Republican.

Matumizi ya makazi ya rais - White House - na Rais Donald Trump na mkewe Melania Trump kwa matukio yanayohusiana na mkutano mkuu wa chama cha Republican unaofanyika kwa siku nne wiki hii, ni halali, kulingana na maafisa wa serikali ya Marekani.

Kwa wengine wanaofanya kazi White House na kwenye utawala, hata hivyo kuna mistari isiyopaswa kuvukwa, kwa mujibu wa sheria inayojulikana kama Hatch Act, sheria ya serikali kuu ya mwaka 1939 ambayo inadhibiti viongozi wengi wa serikali kujiingiza katika shughuli za kisiasa wanapokuwa kazini.

Maafisa wa utawala wa Trump wameonywa kwa kuvunja sheria ya Hatch mara 13 na wachunguzi wa serikali kuu katika ofisi ya sheria ya serikali. Matukio yasiyopungua 12 ya uchunguzi yanaendelea, kulingana na vyanzo ndani ya ofisi ya rais na makundi yanayofuatilia sheria.

Melania Trump, mke wa Rais Trump anatumia bustani ya Rose Garden iliyofanyiwa ukarabati katika viwanja vya White House, kama mahala anapotolea hotuba yake ya Jumanne ya moja kwa moja kwenye mkutano mkuu wa chama cha Republican, ambao ulimuidhinisha rasmi Rais Donald Trump hapo Jumatatu, kuwania tena muhula wa pili madarakani.

Umbali wa mita chache, kumefungwa taa, kuna sehemu imeandaliwa ya wasemaji na pia nafasi ya kutosha kwa watazamaji walioalikwa White House kwa ajili ya hotuba ya Rais Trump ya kukubali uteuzi wake wa chama chake kuwania muhula wa pili kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu. Hotuba ya Trump itafuatiwa na urushaji wa fataki kutoka eneo la bustani ya kitaifa-National Mall.

Afisa wa kitengo kinachosimamia sheria ya Hatch, erica hamrick, alisema katika maandishi hivi karibuni “Rais na Makamu Rais hawafungwi na vifungu vyovyote vya sheria ya Hatch”. Kwa hivyo basi, sheria ya Hatch haimzuii Rais Trump kutoa hotuba yake ya kukubali uteuzi wa chama.

Hata hivyo maandishi hayo hayakuondoa ukosoaji kuhusu matumizi ya White House kwa matukio ya siasa za chama.

XS
SM
MD
LG