Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:10

Hotuba ya Biden bungeni kugusia jukumu la Marekani ulimwenguni


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kujadili lengo lake la kushirikiana na mataifa mengine, na kuchukua jukumu la uongozi katika uwanja wa ulimwengu wakati akitoa hotuba Jumatano usiku kwenye kikao cha pamoja cha Bunge.

Msemaji wa White House, Jen Psaki, alisema kabla ya hotuba kwamba maoni ya Biden juu ya sera za mambo ya nje yatajumuisha “kurudisha tena kiti cha Marekani duniani, thamini zetu ni zipi kama nchi”.

Alisema kuwa rais atazungumza juu ya vipaumbele kadhaa vya sera za mambo ya nje, pamoja na Marekani kujihusisha na China.

Utawala wa Biden unashinikiza kufanya kazi zaidi na washirika, ambapo mwezi huu ilijumuisha kuratibu na wanachama wenzake wa NATO juu ya kuondolewa kwa wanajeshi kutoka Afghanistan.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump

Hii ni hatua ya kuondoka kutoka miaka minne ya sera za kigeni chini ya Rais wa zamani Donald Trump, ambayo ililenga kutanguliza maslahi ya Marekani.

Wakati huo huo, Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi alimwalika Biden kwenye chumba cha Bunge kuzungumza juu ya mtazamo wa kushughulikia changamoto na fursa za wakati huu wa kihistoria”, katika hotuba ambayo inakuja wakati rais anatimiza siku 100 tangu aingie madarakani.

XS
SM
MD
LG