Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:10

Wamarekani waeleza hisia mseto baada Chauvin kukutikana na hatia


Watu wakiandamana Aprili 20, 2021, baada ya afia polisi Derek Chauvin kukutikana na hatia katika kesi mauaji ya Mmarekani Mweusi George Floyd Case Verdict. (Photo by Elijah Nouvelage / AFP
Watu wakiandamana Aprili 20, 2021, baada ya afia polisi Derek Chauvin kukutikana na hatia katika kesi mauaji ya Mmarekani Mweusi George Floyd Case Verdict. (Photo by Elijah Nouvelage / AFP

Hisia mseto zimeendelea kutolewa baada ya afisa polisi wa zamani wa mji wa Minneapolis, jimbo la Minnesota hapa Marekani, Derek Chauvin, kupatikana na hatia ya mashtaka yote matatu.

Chauvin ameshtakiwa katika kesi ya mauaji ya Mmarekani Mweusi George Floyd, karibu mwaka mmoja uliopita.

Baada ya kusikia hoja za kufunga kesi hiyo Jumatatu, baraza la mahakama la watu 12 - wakiwemo wazungu sita na watu sita ambao ni weusi au wa jamii nyingine – walichukua saa chache tu kujadili kesi hiyo iliyochukua wiki tatu, kabla ya kufikia uamuzi.

Rais wa Marekani, Joe Biden, na makamu wake Kamala Harris, walielezea kuridhika kwao na uamuzi huo, na kusema kwamba huu ndio wakati wa kupitisha sheria ambazo zinahakikisha usawa katika mfumo wa sheria za Marekani.

Hukumu katika kesi hiyo itafanyika katika miezi miwili, jaji aliyeisimamia amesema. Tangu kesi hiyo ianze, umati wa watu walikuwa wamekusanyika karibu na Kituo cha Serikali cha Kaunti ya Hennepin, ambapo kesi hiyo ilifanyika, na mahali ambapo Floyd alikufa. Walishangilia wakati uamuzi ulipotangazwa.

XS
SM
MD
LG