Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:04

Kesi ya George Floyd kusikilizwa Jumatatu


Usikilizwaji wa kesi kutoka pande zote za utetezi na mashitaka unaanza leo wa shauri la polisi wa zamani wa jiji la Minneapolis, Derek Chauvin ambaye anashitakiwa kwa mauaji ya Mmarekani mweusi George Floyd.

Tukio hilo la mwaka jana lilizusha maandamano kote duniani.

Kesi hiyo ambayo itasikilizwa na watu 12 wanaounda baraza la mahakama wanatarajia kusikiliza ushuhuda katika kesi hiyo inayotarajiwa kuchukuwa mwezi mzima kukamilika.

Afisa huyo wa polisi ambaye ni mzungu amepinga mashitaka yote yanayomkabili yanayohusu mauaji ya mwanaume mweusi George Floyd.

Alijitetea kwa kusema alichokifanya kiliendana na mafunzo ya kipolisi aliyopewa wakati alipokuwa akimkamata George Floyd.

XS
SM
MD
LG