Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:17

Afisa wa zamani wa polisi Derek Chauvin apatikana na hatia kwa mauwaji ya George Floyd


Afisa wa zamani wa wapolisi Derek Chauvin
Afisa wa zamani wa wapolisi Derek Chauvin

Uamuzi uliokua unasubiriwa kwa hamu kote nchini Marekani umetolewa jioni ya Jumanne baada ya Baraza la Mahakama kukutana kwa saa 10 na kumpata afisa huyo mzungu na hatia ya mauwaji ya George Floyd kwa kumwekea goti kwenye shingo yake kwa karibu dakika 10.

Wanaharakati na watu wa tabaka mbali mbali katika mji wa Minneapolis wanasherekea nje ya mahakama ya kufuatia tangazo hilo.

Kutokana na kwamba mara nyingi sana kuanzia miaka ya 1980 kesi kama hizi, humalizika kwa maafisa wa polisi wazungu kutopatikana na hati, basi wasi wasi ulikua umetanda kote nchini juu ya uwamuzi gani utakaotolewa na wajumbe hao 12 ambapo 6 ni wazungu na sita ni mchanganyiko wa watu weusi.

Mapema White House ilisema inafuatilia kwa karibu kabisa kesi hiyo ya Minneapolisi na msemaji wa Ikulu Jen Psaki anasema wanawasiliana na mameya na magavana ili kuhakikisha kuna maandamano ya amani na utulivu.

“Maoni yake rais, ni yale yale ya kutaka kifungu cha kanza cha katiba kuheshimiwa kinachoruhusu maandamano ya amani. na kuandamani dhidi ya ukosefu wa haki ni jambo ambalo kila mmarekani anahaki ya kufanya . lakini daima anasema maandamano ni lazima yafanyike kwa amani”.

Ingawa matokeo ya kesi hii huwenda ikaamua hatima ya jinsi polisi wanavyowatyendea Wamarekani weusi, lakini waendesha mashtaka katika hoja yao ya kufunga kesi siku ya Jumatatu waliwaambia wajumbe wa Baraza la Mahakama kwamba wana jukumu kubwa kuhusiana na mustakbal wa sheria hapa nchini, lakini ni lazima wakumbuke kwamba kwa wakati huu wanapima uzito wa kesi ya mtu mmoja na wala siyo mfumo kamili ya sheria.

XS
SM
MD
LG