Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 14:25

Baraza la mahakama Marekani linasubiriwa kutoa hukumu ya Chauvin


Picha ya George Floyd ikizungukwa na watu wa rangi tofauti huko Minneapolis, Minnesota
Picha ya George Floyd ikizungukwa na watu wa rangi tofauti huko Minneapolis, Minnesota

Mwendesha mashtaka alimshutumu Chauvin kwa kumuua Floyd m-marekani mweusi kwa kumuwekea goti shingoni kwa zaidi ya dakika tisa. Wakati huo huo wakili wa utetezi alidai Floyd alikufa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya

Baraza la mahakama Marekani linaanza tena majadiliano Jumanne katika kesi ya mauaji inayomkabili ofisa wa zamani wa polisi wa mji wa Minneapolis kwenye jimbo la Minnesota, Derek Chauvin, ambaye anatuhumiwa kumuua George Floyd katika moja ya kesi kubwa nchini Marekani katika miaka ya karibuni.

Baada ya kusikia hoja za mwisho Jumatatu jopo la watu 12 katika baraza la mahakama lilikutana kwa saa nne wakati walipoanza mchakato wa kufanya kazi kuelekea uamuzi. Wakati wa hoja za mwisho Jumatatu mwendesha mashtaka alimshutumu Chauvin kwa kumuua Floyd m-marekani mweusi kwa kumuwekea goti shingoni kwa zaidi ya dakika tisa.

Derik Chauvin, ofisa wa zamani wa polisi anayeshutumiwa kwa kifo cha Floyd
Derik Chauvin, ofisa wa zamani wa polisi anayeshutumiwa kwa kifo cha Floyd

Wakili wa utetezi alidai kwamba Floyd alikufa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya na kwamba Chauvin alifuata mafunzo yake ya polisi alipomkamata Floyd hapo Mei mwaka jana kwenye kona ya mtaa mmoja huko Minneapolis.

Mwendesha mashtaka Steve Schleicher alitoa muhtasari wa kesi dhidi ya Chauvin, afisa wa zamani wa polisi mzungu ambaye alimlaza chini Floyd akiwa na pingu kwenye barabara moja ya mji huo huku Floyd akishtuka mara 27 kulingana na video za kukamatwa kwa Floyd na kwamba alishindwa kupumua.

XS
SM
MD
LG