Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:27

Kesi kuhusiana na kifo cha Floyd yaendelea kusikilizwa Marekani


USA, Minneapolis, Afisa wa zamani wa Polis Minneapolis Derek Chauvin akiwa amekaa mbele ya picha ya George Floyd wakati kesi ikiendelea mahakamani.
USA, Minneapolis, Afisa wa zamani wa Polis Minneapolis Derek Chauvin akiwa amekaa mbele ya picha ya George Floyd wakati kesi ikiendelea mahakamani.

Mahakama moja katika jimbo la Minnesota nchini Marekani inaendelea Alhamisi kusikiliza kesi ya Derek Chauvin, afisa wa polisi, aliyeshtakiwa kuhusiana na kifo cha George Floyd 2020.

Kifo cha Floyd ambacho kilisababisha maandamano yaliyoenea dhidi ya ukatili wa polisi na ubaguzi wa kimfumo.

Wajumbe wa mahakama Jumatano waliona kiasi cha dakika 20 za video ya kamera ya mwilini mwa polisi ambayo ilionyesha muda ambao polisi walipo karibia gari la Floyd na wakati alipopakiwa kwenye gari la wagonjwa.

Video mojawapo iliyochezwa Jumatano ilionyesha Chauvin akisema Floyd alikuwa mtu mwenye umbo kubwa na labda ametumia kitu.

Chauvin alipiga goti kwenye shingo la Floyd kwa dakika 9 na sekunde 29 wakati Floyd akilia mara kwa mara kwamba hakuweza kupumua.

Chauvin, ambaye ni mzungu, alifukuzwa kazi na idara ya polisi ya jiji hilo siku moja baada ya Floyd, Mmarekani mweusi kufariki dunia akiwa chini ya ulinzi.

XS
SM
MD
LG