Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:21

Biden awakutanisha viongozi wa dunia


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais Joe Biden wa Marekani amewaalika Alhamisi karibu viongozi 40 wa dunia katika mkutano kupitia mtandao, ikiwa ni siku ya kulinda mazingira duniani, kwa lengo la kujadili mabadiliko ya hali ya hewa.

Watetezi wa mazingira wanasheherekea mkutano huo wakisema Biden ana fungua ukurasa mpya unaoirudisha Marekani kwenye jukwa la kimataifa baada ya utawala uliotangulia wa Donald Trump kuiondoa Marekani kwenye mkataba wa Paris.

Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

Siku ya kwanza tu baada ya kuchukua madaraka Rais Joe Biden alitaka kuonyesha dhamira yake ya kulifanya suala la mabadiliko ya hali ya hewa kuwa juu katika ajenda yake ya kazi.

Rais Biden anaeleza : Tutajiunga tena na mkataba wa Paris juu ya hali ya Hewa kuanzia hii leo.

Mtaalamu wa masuala ya hali ya hewa katika taasisi ya World Resources David Waskow amesema, mkutano huu wa kwanza wa ngazi ya juu kabisa unaoitishwa na Biden juu ya mabadiliko ya hali ya hewa unataka kuwaonyesha viongozi wa dunia kwamba mambo yamebadilika Washington, baada ya utawala wa Trump kulipuuza suala hilo kwa miaka minne.

Waskow, ambaye ni mtaalam katika taasisi ya World Resoures anaeleza : "Hii ni nafasi kwa Marekani kujitokeza na kujionyesha kwamba imerudi kwenye jukwa la dunia na inalichukulia suala la mabadiliko ya hali ya hewa kwa dhati kabisa."

Alipokuwa anazindua ripoti ya 2020 juu ya hali ya hewa duniani siku ya Jumatatu pamoja na katibu mkuu wa shirika la hali ya hewa duniani Petteri Taalas, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres , amesema huu ndio mwaka wa kuchukua hatua kuwalinda watu dhidi ya athari mbaya kabisa za mabadiliko ya hali ya hewa.

Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres

Guterres ameeleza : "Uharibifu kutokana na hali ya hewa unaendelea kwa wakati huu. ninamhimiza kila mtu kuchukua ujumbe wa ripoti hii kwa dhati. Hebu tu ahidi kuchukua hatua za dhati kustawisha mazingira yetu na kukomesha vita dhidi ya mazingira hayo.

Wanasayansi wanasema ni dhahir athari ni kubwa na tayari zinaonekana na kuongezeka kutokana na mafuriko makubwa, kuongezeka moto wa misitu, ukame wa muda mrefu na vimbunga vikali.

Rachel Cleetus mkurugenzi wa sera za hali ya hewa katika chama cha wanasayansi wenye hofu kuhusu mazingira, anasema tunakabiliwa na hatari kubwa.

Cleetus ameeleza : "Tuna shuhudia kuendelkea kuongezeka kwa joto. tuna shuhudia uongezeka kwa uchafu wa hewa na kuelekea njia tofauti na ile tunayoitaka. na hiyi ndio mana wengi wetu tuna taja muongo huo ni wa mambo kutendeka au kuharibika.

Wanaharakati wanatoa wito kwa Rais Biden kutangaza kwamba Marekani itapunguza kwa asilimia 50 uchafuzi wa hewa ifikapo 2030.

Naye Biden ameshaanza kampeni ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na miradi aliyotangaza kwenye mpango wake wa kuimarisha miundombinu utakaogharimu dola trillioni 2.3 ukiidhinishwa na bunge.

Tayari Warepublican wanapinga vikali mpango huo wakisema ni ghali mno. Kwa hiyo haiko wazi ikiwa mipango ya Biden itafanikiwa wakati macho ya dunia yanaelekezwa kwa wachafuzi wakuu wa mazingira ikiwemo China inayongoza ikifuatiwa na India, kuona ikiwa watatangaza mipango yao kabla ya mkutano muhimu wa Umoja wa Mataifa mjini Glasgow mwezi Novemba 2021.

XS
SM
MD
LG