Pia wamezungumzia masuala ya Mashariki ya Kati na suala la nyuklia la Iran. Mapema Jumatatu Austin akifuatana na Waziri mwenzake wa Israel Benny Gantz walitembelea kambi ya jeshi la anga la Nevatim ambako alikataa kuzungumzia suala la tukio kwenye kinu cha nyuklia cha Iran cha Natanz.
Iran inaituhumu Israel kwa kufanya shambulio la udukuzi jana Jumapili kwenye kinu hicho chake kikuu cha kurutubisha uranium, na kusababisha umeme kukatika, lakini hakuna habari zaidi zinazojulikana kutokana na tuklio hilo.
Austin ni afisa wa kwanza muandamizi wa utawala wa Rais Joe Biden kutembelea Israel na ziara yake inafanyika wakati nchi hiyo ina adhimisha Jumanne, miaka 73 tangu kuundwa kwa taifa hilo la kiyahudi.
Baada ya ziara yake ya Israel Waziri wa Ulinzi Wamarekani ataelekea Brussels Jumanne kukutana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Antony Blinken kwa mashauriano na mazungumzo na washirika wao wa NATO, juu ya masuala muhimu na nyeti kwa wakati huu.