Kura zikiendelea kuhesabiwa Alhamisi baada ya uchaguzi wa bunge wa Jumanne, si Waziri Mkuu Benjamn Netanyahu wala si wale wanaotaka kumuondoa madarakani wenye viti vya kutosha kuunda serikali.
Uwezekano wa wazri mkuu Benjamin Netanyahu kuunda serkali mpya ya mseto umetoweka baada ya chama cha mrengo mkali wa kulia kukataa kujiunga na ushirikiano wowote wenye chama cha waarabu wenye kufuata misingi ya dini ya Kiislamu.
Chama cha kizalendo cha wayahudi kimetangaza leo kwamba hakitajiunga na serikali ya muungano itakayohusisha chama cha Waarabu cha UAL ambacho kimepata viti vinne na Netanyahu atalazimika kujadili nao kujiunga katika serkali yake.
Uchaguzi huo uliokuwa wa nne katika kipindi cha chni ya miaka miwili ulikuwa kwa sehemu kubwa ni kura ya maoni kuona iwapo Netanyahu anaweza kutawala akiwa anakabilwa na mashtaka ya uhalifu.
Lakini si kambi ya Netanyahu wala ya upinzani uliogawika zilizoweza kupata viti 61 katika bunge la viti 120 vinavyo hitajika kuunda serikali.
Ikiwa asilimia 93 za kura zimekwisha hesabiwa Netanyahu na washirika wake wamepata viti 52 kulingana na viti 57 vya wapinzani wake.
Matokeo rasmi yanatarajwa kesho Ijumaa, na hivyo bila ya kufikia makubaliano na Netanyahu kutoweza kuunda serkali au upinzani kushindwa kuunda serikali Waisraeli watalazimka kupiga kura kwa mara ya tano jambo ambalo halijawahi kutokea.