Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:13

Bahrain inataka mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina kuanza upya


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo wakati wa kikao na waandishi wa habari mjini Jerusalem
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo wakati wa kikao na waandishi wa habari mjini Jerusalem

Waziri wa mambo ya nje wa Bahrain ametoa wito wa kufanyika mazungumzo upya kwa ajili ya amani kati ya Israel na Palestina.

Amesema hayo wakati wa mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, nchini Israel.

Pompeo, ambaye ni mwanadiploamsia wa ngazi ya juu wa rais Donald Trump, hakuzungumzia mgogoro kati ya Israel na Palestina katika ziara yake nchini Israel.

Wapalestina wameandamana kupinga zaiara yake ya leo alhamisi katika biashara za wayahudi katika ukingo wa magharibi.

Waziri wa mambo ya nje wa Bahrain Abdellatif al-Zayani amesema kwamba mkataba uliosimamiwa na Marekani kuhusu ufalme wa Ghuba, na umoja wa falme za kiarabu umeboresha uhusiano na Israel na utaimarisha amani katika mashariki ya kati.

Pomepo hana mpango wa kukutana na viongozi wa Palestina ambao wamekataa kabisa msimamo wa rais Donald Trump kuhusiana na mgogoro kati yake na Israel, Pamoja na kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG