Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:03

Mamia ya wahamiaji kutoka Ethiopia wapokelewa kwa shangwe Tel Aviv


Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu

Mamia ya wahamiaji kutoka Ethiopia Alhamisi wamekaribishwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Tel Aviv nchini Israel kwa shamrashamra za kitamaduni.

Hii ni hatua mojawapo katika kutekeleza ahadi ya serikali ya kuwaunganisha wanafamilia waliotengana kati ya mataifa yote mawili.

Takriban Waethiopia 300 wenye asili ya kiyahudi walishuka kutoka katika ndege ya shirika la ndege la Ethiopia wakiwa na vibendera vya Israel wengi wakibusu ardhi mara baada ya kuwasili wakati wakikaribishwa kupita kwenye zulia jekundu.

Ingawa watu wa familia hizo ni waumini wa Kiyahudi, lakini Israel haiwatambui kuwa ni Mayahudi kufuatana na sheria zake za kidini. Hata hivyo wameruhusiwa kuingia nchini humo chini ya programu maalum ya kuunganisha wanafamilia na ambayo inahitaji kibali maalumu.

Maafisa kadhaa wa serikali ya Israel akiwemo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu walikuwa kwenye uwanja huo kuwapokea, wageni hao waliofuatana na Penina Tamano- Shata ambaye ni Waziri wa kwanza wa Isreal aliyezaliwa Ethiopia.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu aliahidi kutekeleza mkataba huo kabla ya uchaguzi mkuu kufanyika mapema mwaka 2020.

Netanyahu alisema : "Mimi na mke wangu Sara tulitokwa na machozi baada ya kuona ndugu zetu Wayahudi kutoka Ethiopia wakishuka kutoka kwenye ndege wakiwa wamebeba vikapu na kubusu ardhi mara baada ya kutua. Inanikumbusha siku za utotoni. Hii ni hadithi ya kiyahudi.

Kundi moja la kutetea haki za kuunganishwa kwa wanafamilia la Israel linakisia kuwa kuna takriban wayahudi 7,000 nchini Ethiopia wanaohitaji kurejeshwa Israel na ambao wamesuburi kwa miaka mingi.

XS
SM
MD
LG